Red Scorpion Mlamba Chumvi
Alikuja Mchina kijijini akasema anahitaji Paka na atanunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi wanakijiji wakahaha kusaka Paka, Wakawa wanawaleta Paka mchina anawanunua wote alafu anasepa nao.
Wiki iliyofuata Mchina akarudi tena,akisubiri paka waje anunue mwito ulikuwa mdogo akawaambia naona wameadimika, sasa nitanunua kwa bei ya 35,000 kwa Paka mmoja, wanakijiji wanaenda deep zaidi msituni, kamata Paka, leta kwa mchina, mchina akawanunua wote kisha akasepa nao.
Baada ya Wiki tena Mchina akarejea na akasema bado anataka Paka wengine, na Mara hii atanunua kila paka kwa bei ya Laki Moja. Wanakijiji macho yamewatoka, hawana tena paka. Mchina anasema basi nitafutieni kwa bei ya Laki na Nusu kwa kila Paka nitawalipa Mchina akaondoka akasema nitarudi wiki ijayo. Kesho yake inasikika kuwa kuna Mchagga anauza Paka kijiji cha pili, na anauza kwa bei ya Laki Moja tu na hapunguzi bei.
wanakijiji wakawahi faster kwenda kununua Paka wote wa kijiji cha pili. Wakarudi kijijini hawana pesa ila wana Mapaka wakijua watamuuzia mchina faster kwa bei ya laki na nusu, wiki ilipofika Mchina hakutokea Kabisa kwenye kile Kijiji !!!! Infact, yule mchina alikuwa anawakusanya tu na kuwahifadhi kule kijiji cha pili akijua atakuja kuwauza kwa bei ya Laki Moja kwa Kila Paka tena kwa hawa hawa wa kijiji.
Ukisikia Wafanya Biashara wakisema biashara ni Ngumu i hope Utaelewa.