Comments za huh uzi zimeni inspire kufungua uzi kuelezea utofauti wa gari na truck.
Kuna ombwe kubwa sana la uwelewa kwa baadhi ya watu kuwa si kila chombo chenye matairi manne kinachotembea barabarani na kuendeshwa na dereva ni gari(car) ..kwani kuna utofauti mkubwa sana kati ya gari na a truck.
Car/gari ni chombo kidogo cha usafirishaji, kilichoundwa mahususi kwaajili ya kubeba na kusafirisha watu..mara nyingi ni kwanzia watu wawili mpaka watu 7.
Cars huwa na eneo dogo kwaajili ya kubeba bags ndogo ndogo walizonazo wasafiri.
Muundo wa gari (car), huwa hazitumii frame chasis (uni body). Body yake ndo huwa chasis yake na vitu vyote ikiwemo engine hufungwa kwenye body.
Body ya gari ikichoka..ndo kufa kwa gari husika kwani suspension system, matairi, engine yote inategemea uimara wa body ili ziwe still..
A truck ni tofauti kidogo na magari. Haya yako designed kwaajili ya kubeba watu wachache na kiasi kikubwa zaidi cha mizigo.
Ziko optimized kwaajili ya kazi nzito. Haziko luxury sana ila zinaweza kumudu kazi ngumu na hali mbaya ya barabara.
Muundo wa trucks ni tofauti na ule wa magari. Trucks huundwa na uti wa mgongo uitwao solid frame chasis. Frame chasis hii ndoyo hufungwa components zote za gari ikiwemo suspension system. Engine, body etc. A truck inaweza isiwe na body, na bado chasis pekee ikiwa na componets zake ikiwemo engine...inaweza kuingia barabarani na kutembea vizuri tu..
Hivyo, kwa nature ya trucks ambazo pickup ni lite version yake, mtumiaji huwa hazingatii umri wa gari au namba..ila ni je...does it serve the purpose?
Kuna mtoa hoja amezungumzia bei husika ni heri ya kununua nissan x trial...ni kweli kabisa...ila je? X trial inaweza kwenda kuvuna nanasi pale kiwangwa ...na ikabeba chache kuleta sokoni?
Je ni gharama kiasi gani ungetumia kuchukua cement dukani na kupeleka site kila siku kama una ujenzi.....x trial ingemudu? Umenunua kitanda....unaduka lako la mangi...ni gharama kiasi gani ungetumia kununua bidhaa kurestock duka?
Hivyo basi....pickup trucks si gari ya kila mtu....ni gari ya mkandarasi...ni gari ya mkulima..ni gari ya mjasiriamali na ni gari ya mfugaji na ni tumaini kwamba kundi hili la watu wao wanajua thamani ya trucks. Trucks ni gari zinazolala porini kujenga barabara ili x-trial ipite..ni gari inayopeleka Sembe dukani ili mkeo anunue akusongee ugali nyumbani. Its not a vehicle for every one.
Kuhusu bei ya mleta mada...siwezi kugusia ilo...ni biashara yake ila nimeattach gharama za befoward za hilux model hii ya 1990...kufanya short comparisons....
Ni kwamba thamani ya truck model hii bado haijashuka thamani kama wengi wetu tunavyo dhani.