Navalny: Documentary ya mpinzani wa Putin yashinda tuzo ya Oscar

Navalny: Documentary ya mpinzani wa Putin yashinda tuzo ya Oscar

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Jana ulikuwa usiku muhimu kwa ulimwengu wa sanaa ya filamu duniani. Tuzo kubwa na maarufu zaidi duniani katika sanaa ya filamu za Academy au maarufu kama Oscar Awards zilitolewa kwa washindi mbalimbali kwa vipengele 24 huko Hollywood, Los Angeles, California.

Katika kipengele kimojawapo cha documentary bora ya mwaka 2022 tuzo ilienda kwa Navalny ambayo ni documentary inayoelezea maisha ya mpinzani mkubwa wa Putin kisiasa kuwahi kutokea Russia na aliyegoma kwenda uhamishoni nje ya Russia baada ya kulishwa sumu, Alexei Navalny kwa sasa yuko katika kifungo kirefu gerezani kwa makosa chungu nzima yaliyotengenezwa.

Director wa Documentary ya Navalny ni Daniel Roher kijana Mcanada wa miaka 30.

Iko katika lugha ya Kirusi na Kingereza. Documentary hii dirisha lingine kubwa kupitia sanaa kuweza kuchungulia ndani ya utawala wa miongo miwili wa wa kiimla wa Vladmir Putin.

=======


Trailer ya Navalny
 
Hizo ni tuzo huru, zinaandaliwa na makampuni/mashirika binafsi kwa mchakato wa wazi wa uchambuzi na kura kutoka kwa wataalamu na magwiji wa filamu
Bila shaka ingeshinda maana watoaji tuzo ndio hao hao wasiompenda putin.
 
Hizo ni tuzo huru, zinaandaliwa na makampuni/mashirika binafsi kwa mchakato wa wazi wa uchambuzi na kura kutoka kwa wataalamu na magwiji wa filamu
Mkuu hakunaga ubinafsi wala nini ndio maana kuna kampuni zimezuiwa kufanya kazi na serikali za china na Iran wakati ni kampuni binafsi.

Kwanza media industry hasa filamu ni chombo cha kusambaza propaganda na tamaduni zao.
 
Kipengele kilichomshindisha kitakuwa ni hicho cha upinzani na Putin
 
Huyo Navaly ndo Nationalist kuliko hata Putin...huyo akipata nafasi kuna vinchi vitaimba aleluya...kwanza aliunga mkono Crimea kwenda Urusi...
 
N yajiandaa kutoa movies nyingi kutokana na vita ya Ukraine
Ndo walichobakiza,maana hawana story siku hizi,Iraq,Syria, Afghanistan washamaliza story zake,Sasa Ukraine na chumvi nyingi humo ndani
 
Back
Top Bottom