Navyomkumbuka Edward Moringe Sokoine-alijiuuzulu Uwaziri Mkuu ili kwenda kusomea degree ya masters Yugoslavia

Navyomkumbuka Edward Moringe Sokoine-alijiuuzulu Uwaziri Mkuu ili kwenda kusomea degree ya masters Yugoslavia

EngutanK

Member
Joined
May 3, 2021
Posts
99
Reaction score
244
Alijua wazi kabisa huwezi kufanya mambo mawili magumu kwa wakati mmoja, akaona aache cheo kikubwa kabisa cha uwaziri mkuu ili kwenda kutimiza adhima yake ya kujiendeleza kielimu huko nchini Yugolavia ya wakati ule.

Wanzetu hawa utaona leo ni waziri na kesho amedoctorate sasa huwa utafiti wanafanya wakati gani na uwaziri wanafanya wakati gani mbona mwenzaoSokoine alishindwa kufanya mambo wawili kwa wakati mmoja?

Tunarudi kule kule kwenye elimu ya vyeti faki, mawaziri kuwa na shauku ya kudoctorate inawahamasisha na wengine nao kutaka wadhifa wa U docta, ili aitwe doctor fulani, inafanana kabisa na mtu mmoja kwenye basi akiomba basi lisimame akachimbe dawa basi basi lote abiria wanashuka kuchimba dawa. Sasa hawa mawaziri waliodoctorate wakiwa kazini wanahamasisha na mawaziri wengine waliobasi waunge tela basi bunge zima watakuwa madocta mwisho wa siku.
 
Hii nchi tuiache hivi hivi,

Edward Moringe Sokoine, nilikulilia japo sikuwa na ufahamu mkubwa.

Edward Moringe Sokoine ulifunga bunge pale dodoma, ukasema tuonane kikao kijacho, siyo kosa lako uliposahau kusema Mungu akipenda tutaonana, pengine ulisema serikali haina dini, japo Mungu ni wa wote.

Ukafika njiani hapo gari ikakuparamia, ikiendeshwa na dogo mkimbizi, uso kwa uso.

Wakasema hukuishia pale ila ilitumika nguvu kubwa sijui vizuri ni muda sasa umepita.

Ukazikwa huko kwenu, ikapita miaka mingi wakasema inabidi mwili uhamishwe pale kwani boma lilihama, sijui iliishia wapi.

Nilikulilia Edward Moringe Sokoine

Sasa uko huko Mbinguni, je Mwalimu Nyerere mnaonana?

Ninayo mengi ila mengine ni magumu ngoja niishie hapa.
 
Back
Top Bottom