ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Wakuu ona Mimi nikiwa kijiweni kwetu stori zangu nyingi huwa Ni za kutoka JF.Nawaambiaga masela kuwa Mimi nafahamika Sana jf.ona nawaambia kila member kutoka sehem mbalimbali ndani na nje ya nchi ananijua.nawaambia maisha ya humu ndani tunachati na watu wakubwa vigogo mashuhuri na watu maarufu.afu washikaji nikiwa nawahadithia wanatulia kimya wananisikiliza wakitaka kujua jinsi ya kujiunga nawaambia haiwezekani Ni kazi Sana waendelee tu kuwa wasomaji.nawaambia kwamba humu ndani tunapiga stories na Hadi wabunge bila kujijua.nawachota akili na kuwashika masikio usisahau nawaambiaga kila siku mimi naingiza buku 7 zinatumwa kutoka ikulu kumbe uongo.yaani kiufupi Mimi mwongo mwongo Sana nikiwa humu mwongo nikitoka nje ya jf mwongo Kali kuliko zote Ni hii kuwa Mimi Nina hisa jamiiforum afu Sasa kinachonishingaza wananiamini asee kweli usilolijua Ni sawa na usiku wa giza.