Nawahurumia sana viumbe hai ninapowakuta kwenye matatizo

We saidia tu sababu kila mtu ana jambo lake ambalo likiwekwa wazi au ukifikiria kwann anafanya unaona ni tatizo tu la akili.

kuna wanaozungumza na watu wasioonekana,

kuna ambaye akiona kioo anaanza kufanya vituko,

kuna wanaojirikodi wakiimba huku wanabinua mdomo,

kuna wanaorikodi dashbord ya gari ikiwa na mziki na kuweka status huku kila saa akiview wangapi wameona dashbord n.k n.k
 
Kuzungumza na watu wasioonekana imenitokea sana!!usikariri
 
Reactions: Tsh
Kuzungumza na watu wasioonekana imenitokea sana!!usikariri
Hilo ni jambo lako mm nilikariri la nn?

Mm nimesema kila mtu na jambo lake ambalo kwa mwingine ukilifikiria analiona kama tatizo la afya ya akili.

Kama huwa unazungumza na wasio onekana endelea tu na vikao vyenu.
 
Hii dunia ina mambo ya ajabu sana. Mfano mimi ni baba zima na midevu yangu na nina mke na watoto, ila naogopa KUKU balaa..! Yaani nipo radhi nipambane na simba, chui, nyati, dubu nk lakini KUKU nikimuona tu miguu inagongana yaani naishiwa nguvu kabisa siwezi kumsogelea wala kumshika na akinifata natoka nduki kali..!
 
Laiti ungejua mbu wanavyotusumbua usiku hata usingewaonea Huruma
 
Endelea kuishi hivyo mkuu siyo kila mtu hupenda vitu vinavyomzunguka
Ninaimani tulipewa akili ya kuvitawala viumbe vya ardhini na majini wala siyo nguvu ya kuviangamiza
 
kuongea na wasionekana inakuwa vipi
Unakuta tu Kuna sauti inakuja inakuongelesha, mnaongea , sauti unaisikia lakini huoni mtu mara nyingi ni mizimu ya kwenu huko!
Unaweza kuagizwa ufanye hivi au vile!!
 
Hivyo ndivyo wanadamu tunapaswa kuwa......bahati mbaya tunaishi katika Dunia iliyojaa unyama mpaka WEMA unaonekana jambo la ajabu sana..........

Ulimwengu tulionao waungwana na wema hawapendwi bali wanatumiwa na wanaojua kuyatumia hayo madhaifu hayo.......ndio maana nyakati hizi watu WEMA wanaonekana wajinga na wasiojielewa na watu wabaya wanaonekana wajanja........

Ukiokota mali ya mtu ukamtafuta mwenyewe utaonekana boya hata Kwa mkeo au mumeo lakini ukiificha utaonekana mjanja.,......
 
Pamoja na moyo wote huo, ukiulizwa umesomea nini si ajabu umesomea ufundi redio...

Nenda kasomee mambo ya wanyama Mweka, uwe hata zoo keeper...
 
Mm mpaka wanangu nimeshawakataza km mdudu hana madhara kwako kwa nn umuue maana waswahili tuna ujinga mwingi sana wadudu wana mishe zao ww unaenda kuwakanyaga ama kuwaua bila sababu maalumu huu mm hua naona ni ukatili
 

Ni jambo jema na Huna shida, ila jifunze kwamba huwezi control mazingira yote, kaa kwenye eneo lako la ubinadam na binadam wenzako.
 
Pamoja na moyo wote huo, ukiulizwa umesomea nini si ajabu umesomea ufundi redio...

Nenda kasomee mambo ya wanyama Mweka, uwe hata zoo keeper...
kama ulijua vile, lakini bado sijachelewa kurudi kwenye lane yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…