Nawakumbusha umuhimu wa kuchangia kwa umakini na heshima katika mijadala

Nawakumbusha umuhimu wa kuchangia kwa umakini na heshima katika mijadala

Habari wanajamii,

Napenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha baadhi ya wachangiaji umuhimu wa kuchangia kwa umakini na heshima katika mijadala mbalimbali inayowasilishwa hapa Jamii Forum.

Tunaposhiriki katika mijadala yenye maswali au changamoto zinazohitaji mawazo ya kina, tunapaswa kuelewa kuwa watoa mada mara nyingi wanategemea majibu yenye msaada na yanayoendana na maudhui ya swali au changamoto zao.

Masihara yasiyofaa au kuchangia mambo yasiyo na maana katika mada muhimu kunavunja moyo watoa mada na kupoteza lengo la majadiliano.
Hii inaweza pia kudhoofisha hadhi ya jukwaa letu kama sehemu ya kupata msaada wa kweli na kubadilishana mawazo yenye manufaa.

Naomba tushirikiane kwa heshima, uelewa, na nia njema ili kila mmoja ajisikie kuthaminiwa na kupata msaada anaoutafuta.

Kama hatuna cha kusema kinachofaa, ni bora tusichangie/kaa kimya.

Ni matumaini yangu kuwa wenye tabia hiyo watabadilika ili jukwaa hili liwe na manufaa ya wote.
Sawa,ila kuna mizaha chanya,yenye kufurahisha na kufungua Akili!.
 
Back
Top Bottom