Nawakumbusha wote walioenda kupaka majivu jana, mfungo umeanza!

Nawakumbusha wote walioenda kupaka majivu jana, mfungo umeanza!

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2022
Posts
4,114
Reaction score
6,449
Rejea kichwa cha mada hapo juu.

Nawakumbusha wale wote walioenda kupaka majivu jana na jana walianza mfungo ila leo wanaendeleza yaleyale ya hapo kabla na wanasema wamefunga mfungo wa Kwarezima, sasa wewe unasengenya, unawasema wengine vibaya, huonei wengine huruma, husaidii wengine, nk unafunga nini sasa?

Nakuuliza wewe hapo unafunga nini maana unayafanya yale yale tu ya siku zote nini unachofunga?, si bora usingeenda hata kupakaa majivu, hivi mnafikiri kupakaa yale majivu ni fashion? Jana umezunguka kila mtu akuone umetoka kupaka majivu leo umeamka unaanza tabia zako zile zile umesahau upo kwenye kipindi cha mfungo wa Kwarezima?

Umeenda kupakaa majivu ila sababu domo lako ni chafu domo limezoea kuongea maneno maovu maneno machafu maneno yasiyo na tiba leo umeweka kijiwe na wenzio unaanza kumsema na kumsengenya mtu mwingine huyu vile huyu mara huyu vile huyu kafanya hivi huyu hafanyi hivi, umesahau jana ulienda kupakaa majivu wewe au ulienda kupakaa km urembo?

Meseeji sent & delivered.
Muwe Kwarezima njema.
Kalamu imeisha wino....
 
Kufunga siyo mchezo.
Utawsikia wasiofunga waakwambia " wateja wa ..... kit moto wamepungua" hii siyo kweli bali ni kutafuta justification ya kutofunga
 
Kufunga siyo mchezo.
Utawsikia wasiofunga waakwambia " wateja wa ..... kit moto wamepungua" hii siyo kweli bali ni kutafuta justification ya kutofunga
Hio sababu wanatumia wa kwaresma au wale wa mwezi mtukufu
 
Sina hakika ila ninachojua siyo kweli! Mbona wateja wa soda hawapungui??
halafu ngoja kwanza leo niende kwa mangi nikaagize au nisikilizie kabsa wiki ijayo nicheki bei na ujazo wanaoweka kwa sasa ukoje ........soda si zinanyweka baada ya kufuturu au mida ya daku tena sahv hata mauzo ya soda yanaweza yakawa yamepanda hasa kwa dar ile mida ya jioni
 
Back
Top Bottom