Nawaomba mniombee msamaha kwa mke wangu!

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Posts
6,781
Reaction score
1,647
Natubu kwa MWENYEZI MUNGU NA KWA MKE WANGU, NAMWOMBA SANA ANISAMEHE. nilimwoa mke wangu nikiwa sina chochote na kwa msaada wake wa mawazo na msaada wa Mungu tulifanikiwa kujijenga kimaisha na hali yetu ya kipato ni nzuri kidogo. nashindwa nieleze vipi ila ninachojua nimemkosea sana mke wangu na baadhi ya makosa yangu BAADA YA KUPATA MAFANIKIO NILIANZA KUMDHARAU SN MKE WANGU na kwa muda mrefu nimekua nikishirikiana na ndugu zangu kumnyanyasa na kumtukana mke wangu kwa makusudi mara nyingi nimewahi kulala nje ya ndoa nikiwa na wanawake wengine akiwemo ndugu yk wa karibu sn na mke wng alijua yt,kwakweli nimemfanyia mabaya mengi sn na amekua akilia na kusononeka sn lkn bado alinionyesha upendo na baada ya kuona kila ninachomfanyia haondoki siku 1 NILIMTUKANA SN bila sbb na kumfukuza kama mbwa, wakati anaondoka aliniambia "MUME WANGU NILIKUPENDA SN ZAIDI YA NILIVYOIPENDA NAFSI YNG, UMEAMUA UNINYANYASE NA KUNIFUKUZA KAMA MBWA, NAENDA LKN UTANIKUMBUKA SN NA SITAKAA NIRUDI KWAKO MILEE"
 
Mbona unatupa story nusu nusu; kipi kimekukuta mpaka umeanza kumkumbuka kama alivyonena.:juggle:
 
Hebu nitumie namba yake ya simu, kuna mjomba wangu shaba anasaka kwa udi na uvumba mwanamke mwenye tabia njema na mvumilivu, amuoe kwa gharama yoyote amuoe na ampe mapenzi yake yote.
 
alipomaliza kusema hayo alibeba mtoto na kuniaga kuwa anaenda na kuniambia kila nilichochuma naye ameniachia kama zawadi, ni miezi imeisha nateseka sana sioni mke wl mtoto nimeenda kuomba msamaha amekataa kurudi, nimetuma washenga waniombee amekataa kurudi nyumbani, ndugu jamaa na marafiki wamemsihi arudi kwake amekataa katakata, NAOMBENI MNISAIDIE NANYIE KWANI NIMEGUNDUA KUWA MKE WANGU ALINIPENDA TOKA MOYONI NA SITAKAA NIPATE MKE KAMA YEYE TENA. NISAIDIENI~ ~.
 

too hypothetical hebu tuambie wataka tuongee na mkeo akiwa wapi na vipi? Mtu wa kwanza kwenda kumwangukia ni mkeo. umemkumbukia nini sasa ivi?
 
Ukiona hvyo ujue walimwengu washamfunza aise. Kama uliweza kufanya yte hayo bc hukuwa/huna utu ht kdg. Pesa inakupa jeuri wkt ww c lolote c chochote. Nawachukia sana watu wa namna yako.
 
Pole sana,ndio ujifunze kuwa mwanamke anaumuhimu wake!!
 
too hypothetical hebu tuambie wataka tuongee na mkeo akiwa wapi na vipi? Mtu wa kwanza kwenda kumwangukia ni mkeo. umemkumbukia nini sasa ivi?
ni mwana jf mwenzetu na moja kati ya 2 ya id zake ni "lonely heart"
 
JF bana...huyu Super Luimbo anaweza akawa ndo Klorokwini na nyi msijue. Wenyewe mnajipinda kutoa ushauri huku yeye akiangua vicheko tu huku akiwachora! KANUSHO: Sisemi Super Luimbo ndiyo Klorokwini.
hapana mimi sio klorokwini MIMI NI SUPER LUIMBO wala sina id nyinine
 
Yani hukua na hisia hata moja kama mlitoka mbali nae? wewe hata akirejea tena unamchokoa roho au mara hii utamua kabisa loh fisadi wa roho yako mwanamme weye, yani ulipokua ukimfanyia mabaya hata nafsi yako haikusuti? ushaangukia pua sasa unamtafuta si umemfanyia visa vya nuhu na Firaauni bado hujaridhika sasa unataka roho yake ndio mana unamrejesha? ebu tafuta fisadi mwenzio mtakae fanana huyo hakufai hujui kama UNAEOKOTA NAE KUNI NDIO UNAEOTA NAE MOTO? loh asara yako....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…