Nawaomba Simba wamsajili Frank Domayo, azam wamemuaga leo

Nawaomba Simba wamsajili Frank Domayo, azam wamemuaga leo

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Mimi bado naamini kiungo Frank Domayo bado ni fundi hasa wa mpira hasa anapocheza kiungo wa chini, Domayo ambaye alipatwa na majeraha sana kiasi kwamba Azam walimpeleka Afrika Kusini kwa matibabu.

Leo Azam wameandika kwenye ukurasa wao kuwa msimu ujao hawatakuwa naye tena.

Mimi namuona bado Domayo ana ufundi na uzoefu, kuachwa Azam haina maana kuwa Domayo hana uwezo ama amekwisha kisoka, kumbuka azam waliwahi kufanya utoto kama huo kwa kapombe, Manula, Bocco na Nyoni na hadi Leo wanajuta.

Simba ina matatizo makubwa kwa viungo wa chini, Jonas mkude ameshakuwa maji ya jioni, ni kama gari la mkaa, Leo mzima kesho mbovu.

Naamini Domayo ni mzuri na ana uzoefu wa kimataifa.

Nawaomba viongozi wangu wa Simba wampe japo mwaka Domayo, huwezi kumfananisha Domayo na Mzamiru wala Jimmson Mwanuke au Mhilu.

Mtakuja kunishukuru.
 
Huyu si ni mmoja wa wacgezaji waliovimbishwa kichwa na Dauda?

Nashauri Simba itafute wachezaji ambao wako humble na sio hawa wanaooteshwa mapembe na waandishi wa habari hadi wanajiona level za akina Mesi
 
Back
Top Bottom