Nawaomba ushauri ushauri! Wanajamvi

Nawaomba ushauri ushauri! Wanajamvi

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
7,460
Reaction score
4,761
Hivi jamani mama anayanyonyesha may be mtoto ana miezi kadhaa, (3months) akapata mimba nyingine afanyaje?yule mtOtO mdogo? Na dalili zipi zitaonyesha kuwa mtoto amedhurika na maziwa ya mama yake

pliz pliz pliz ninahitajika nimjibu mtu nanimekosa jibu sahihi,kama hujui usijibu pumba potezea tu ,au matusi sitaki
 
Mama kunyonyesha na kisha kuconceive siyo kitu kibaya kigeni na wala siyo dhambi. atagundua kwa kufanya UPT siku hizi annanunua kajistrip tu anapima mwenyewe.

La kufanya mwanae hawez kamwe kudhurika na maziwa hayo na nashauri aendelee kumnyonyesha hadi ujauzito ufikie miezi 7. kikubwa aongeze upendo zaid kwa mwanae, amkubatie muda mwingi, ahakikishe mtoto ananynya sana na yeye binafsi ale sana vyakula kwa kufuata lishe bora na kamili. Pia aongeze sana kiwango cha usafi wa mazingira na mwili wake. ili kumkwepesha kichanga na maradhi yyte yale. ajitahd sana mtoto asipate mmagonjwa kama kuhara na malaria yatamdhofisha zaid.

ingawa siyo vizuri sana ila kam anaweza aanze kumlikizia huyu mtoto japo uji mwepesi mara moja kwa siku, ajitahidi sana apate maziwa safi ya ng'ombe siyo ya dukani amlishe mtoto 3/4 ya milo ya mtoto iwe ni maziwa.

asiendekeze dalili na maudhi madogo madogo ya mimba na kumsahau mtoto huo ni mwiko.

Mwiaho kabisa mtoto huwaga habemendiki iwapo atatunzwa vizuri. Mwambie mumewe asione ubahili kugharamia sana swala la lishe na usafi
 
Ushauri mzuri sana gfsonwin.
Nivea, zingatia usafi na lishe bora. Usisahau juice fresh na mboga za majani wakati ana umri wa 6months.
 
nashukuru sana sana nitawakilisha wakuu
 
Back
Top Bottom