Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Karata kwa Tanzania zimebaki kwa timu tatu baada ya Azam kuondolewa mashindanoni jana, niliwahi kuelezea hapa namna mashabiki walivyo na nguvu lakini sikueleweka wajuaji wakaniponda sana, APR kule kwao walilazimika kuingiza bure wanafunzi kwa kuwataka wawe na kitambulisho cha shule ndio unaingia bure, we unadhani walikuwa wana maana gani, hawakutaka mapato? No walijua mashabiki wana nguvu sana, uwanja jana ulitapika sio kawaida, mashabiki wana nguvu sana uwanjani, wao wanachangia kwa kiasi kikubwa kutia mishe mishe, kucheza peke yenu bila mashabiki kunawafanya wapinzani wenu wa relax, mpinzani akicheza na wewe bila mashabiki wao anaona kama yuko neutral ground, hivyo anafurahi, mashabiki wakiwa uwanjani wanahamasisha hata kumtia presha refa, jana goli la pili la APR lilikuwa clear offside lakini kwa sababu mashabiki walikuwa wengi refa hakuona sababu ya kukataa, alipeta tu.
Kama ukiwa na mashabiki wengi utapata penati, offside zinaweza kuachiwa achiwa kutokana na makelele ya mashabiki, mwamuzi naye binadamu, sasa mwamuzi anachezesha mechi hapigiwi kelele, anajua akipigiwa kelele na benchi la ufundi ni rahisi kuwaadhibu wale wa benchi la ufundi lakini kwa mashabiki hadi awaone au kuwaadhibu wote hawezi.
Tusipuuze mchango wa mashabiki katika soka, Azam ameadhibiwa hapa nyumbani kwa kukosa mashabiki, angetengeneza mkakati wa kubeba mashabiki wa bure pale Chamazi, APR alikuwa anakula hata bao 3, sasa leo Coastal anacheza.
Ana mlima mrefu sana, kumpiga aidha 3 0 waende kwenye mikwaju ya penati au kumtandika bao 4 mpinzani wake, mechi ni ngumu kwa sababu katika mechi za hivi karibuni Coastal hawaonekani kama wana kiu ya kufika mbali, kwanza haina washambuliaji wazuri wanaoweza kubadili matokeo, pili walinzi wao sijui kama wanaweza kuzuia mpinzani asipate bao, Coastal inahitaji sapoti yetu watanzania ili ifuzu michuano hiyo hatua inayofuata, njia pekee ya kumsaidia mdigo huyu wa Tanga ni kwenda uwanjani kuwaunga mkono, wameshasema wenyewe kuwa kiingili miguu yako tu, chonde chonde watanzania, tuache ubinafsi na mambo ya simba na yanga, Azam kashaondolewa nchi imeshapoteza, hajapoteza Azam, nchi imepoteza.
Najua leo Simba anacheza, wengi watakwenda dimbani na wengi wataiangalia kwenye Runinga lakini kiukweli mchango wa washabiki katika mchezo wa leo ni muhimu sana ili Coastal aweze kufuzu, Yanga jana wamejaza uwanja wa Chamazi, sio wajinga, kuna mambo yanafanywa na kamati yao ya ufundi kuhusu mchango wa mashabiki,