Nawaona timu Simba meno thelathini na nje yote mbili

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2014
Posts
3,292
Reaction score
7,867
Baada ya wababe wao Kagera sugar kushuka daraja, ni vifijo na nderemo tu. Ikumbukwe klabu ya Simba haina rekodi nzuri kwa kagera kwa misimu miwili mfululizo.

Msimu wa 2017/2018 mbele ya mgeni rasmi Kagera walitoboa tundu la Simba. Msimu wa 2018/2019, Kagera sugar walitoboa toboa tundu la Simba nje, ndani.

Lakini licha ya kuwa wababe kwa Simba wameshuka daraja wakiwa na point 44 tu. Walimkazia Boda boda fc pekee na wakasahau timu nyingine.

Ngoja nitafakari, timu ya kuipa mikoba ya Kagera ili tundu liendelee kutobolewa.
 
Sijui nani mwingine atakaye tuchapia mikia nje ndani? Daah Kagera walifeli wapi! Natamani Zahera amchukue Mecky kumsaidia;
 
Naona azam anapiga vyura hadi mropokaji kasingizia t- shirt
 
Msimu wa 2017/2018 mbele ya mgeni rasmi Kagera walitoboa tundu la Simba. Msimu wa 2018/2019, Kagera sugar walitoboa toboa tundu la Simba nje, ndani.
... na misimu yote hiyo 2017/2018 na 2018/2019 ni Simba inakuwa bingwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…