Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,290
- 2,468
Ukweli mchungu ni kuwa shamrashamra zikishapungua, mwenyekiti wao bila kificho atawaambia kupitia umma kuwa sasa ni wakati wa kulipa fadhila. Haiingii akilini uwang'oe Mdee, Mbowe, Lema, Mbilinyi, Bulaya, Heche, Matiko, Msigwa na usilipe fadhili (price to pay).
Jiandaeni kisaikolojia. Jiandaeni kutumika kama pampas ndani ya chama chenu hicho hicho. Jiandaeni kufungwa midomo. Jiandaeni na utumwa huru.
Najua wengi nafsi hazina kicheko japo kinywani vipo. Dr. Tulia kasema mwenyewe hawakustahili. Sio kauli ya kubeza tu. Wameona uhalisia na sasa wanashangaa
Ni kama Yuda aliyetamani kuvitema vipande vya fedha ikashindikana kwa kuwa ilibidi maandiko yatimie, ila ole wake ambaye maandiko yametimia kwa njia ya yeye.