Mwl Ngasa
Member
- Aug 9, 2012
- 32
- 7
Siku zote nimekua nikisikia kuwa waislam wanaonewa,wanahujumiwa, wananyimwa haki zao, wanadhulumiwa sasa kwa hapa tz sijui hata nijieleze vipi kwani mfumo wa maisha na imani zao ndo unaowapeleka huko wanapotaka kuwa. Mimi nina ndugu zangu kwenye familia ni waislam na sisi ni wakristo sasa lipokuja swala la Elimu hususani Elimu ya sekondari naona wenzetu wanashule duni sana tena nidham za shule zao ni mbaya hata kufikia wanafunzi kuishi maisha duni kielimu haf bado wanapeleka watoto wao huko, wanapofeli yani hata hawashtuki wanasema wanaonewa na NECTA! Hiyo necta ndo inasimamia nidhamu mashuleni? Hapa tz shule nzuri zote ukifanya tathmin uzuri wwte ule uwe wa majengo, walimu, kufaulisha au vifaa vya kufundishia lazma uambatane na NIDHAM ya wanafunzi ndo inayo vuta usikivu! Jamani inawezekana kweli huko mlikotoka mlikuwa mnaonewa lakini kwa hapa mlipo eneo la Elimu mnalifanyia nini? Chuo kikuu chenu kimoja wenzenu wanavyo takribani kumi na saba, Je mko serious kweli! Baada ya miaka ishirini mbele ajira itakuwaje kama taaluma ya vyuo ikifuatwa? Kwasasa kiukweli bila kuliangalia kwa namna ya pekee swala la Elimu ndugu zangu hali ya ajira kwa siku za usoni italeta shida! Sijui kama hapa kwenye eneo la Elimu kunahujuma wala sijawahi kuona, ninazaidi ya miaka kumi kazini kama mwalimu nikifundisha wanafunzi wote waislam na wakristo sijawahi kupoteza mwanafunzi eti kafeli kwa dini yake hilo hakuna kabisa!