Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Yanga wana timu nzuri sana na hata jana tumeona licha ya kuwa wamefungwa wakiwa pungufu lakini Azam waliomba poo, mimi ni mtu wa mpira siongelei mpira kiushabiki ama kutafuta followers, nimekaa kwenye tasnia ya soka la bongo tangu mwaka 1989 nikiwa naingia bure uwanja wa uhuru, enzi hizo Sigara vs Pilsner ndio derby, Nyota Nyekundu vs Simba, kulikuwa na akina Pamba, Tukuyu, Ushirika ya Moshi ya akina Kaunda Mwakitope, Venance Mwamoto, Mecco, Reli ya Morogoro ya akina Mohamed Mtono, Fikiri Magoso, Duncan Butinini, Mirambo ya Tabora nk.
Kwahiyo sibahatishi napoongelea mpira, huwa kuna wakati nainjoy sana yule mtangazaji wa Azam Mahmoud Zubeiry anapowafanyia mahojiano akina Innocent Haule, Joseph Fungo, Edgar Fongo, Hamza Maneno, Zamoyoni Mogella, ananikumbusha mbali sana.
Kwahiyo Yanga wana timu nzuri na uongozi wao pia licha kuwa una makandokando mengi lakini wanajitahidi sana kuficha makandokando yao, kwa mfano mimi sikubaliani na madeni ya kijinga kijinga ambayo Yanga inadaiwa na wachezaji wa kimataifa, leo GSM wakiiacha Yanga itakuwa kiama pale, ataacha madeni na klabu inaweza kufilisiwa, wengi wanaona timu inashinda wanaona sawa tu.
Sasa kuna hili hapa, kwa sasa ndani ya Yanga kuna mgogoro baina ya wazee na Rais wao, ugomvi wenyewe umetokana na na Rais alipoamua kuipeleka timu kule kwenye uwanja wa KMC na kucheza mechi za kirafiki kadhaa, wazee walimshauri Rais wao asipeleke timu kule na kwamba uwanja wa Chamazi unatosha, walimwambia wao wanaijua Simba kwa sababu wanaishi nayo tangu mkoloni, walimwambia Simba sio Kuku, hata kuwafunga tunawafunga lakini kazi kubwa inafanyika na ndio maana tunatumia njia nyingi kuingia uwanja wa Taifa hadi tunapigwa mafaini yasiyokuwa na sababu, yote ni kukimbia mitego ya hawa watu.
Sasa kule uwanja wa KMC kuna mipango ya Simba kule, dua na mambo mengine mazito yamefanyika kule, Rais aligoma na akawa anapeleka timu kule Mwenge kucheza mechi kadhaa za kirafiki.
Sasa tangu waguse ule uwanja wachezaji watatu wamenasa kwenye ulimbo wa Simba, Halid Aucho, Prince Dube na Azi Ki.
Hawa wachezaji viwango vimeshuka kwa sababu wameingia kwenye gidamu na yote wazee wa klabu wanadai ameyataka Rais wao, kwa sasa wanapambana sana kuondoa ulimbo huo ili warudi kwenye mstari.
Kwahiyo ni kweli Aucho, Dube na Aziz wameshuka na hiyo ni kutokana na kuingia kwenye ramani ya vita ya wazee wa msimbazi.
Ni kama sisi walivyotufanyia kwa Mutale, Mukwala, Ahoua na sasa wamemfanyia Ateba.Msione hivi jamani kuna mengi sana ndani ya hizi timu.Chukua hii.