Nawapongeza Baraza la mitihani(NACTE) kwa kufuta machaguo kwenye mitihani wa hisabati.

Nawapongeza Baraza la mitihani(NACTE) kwa kufuta machaguo kwenye mitihani wa hisabati.

NgerukeAbra

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
1,336
Reaction score
2,008
Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) limefanya mabadiliko kwenye mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kwa kuondoa machaguo ya majibu kwenye somo la hisabati kuanzia mitihani ya mwaka huu.

Pia wanatarajia kufanya mabadiliko kama haya kwa ngazi ya sekondari kwenye masomo ya Fizikia, Kiingereza na Baiolojia.

Dah hii ishu ya multiple choices kwenye hisabati ilikuwa inaniboa sana!
 
Kama ya kuchagua jibu sahihi hawawezi je kukotoa wataweza? Watoto watafeli vibaya itabidi standardize ihusike kuinua maksi vingenevyo spoon feeding itatumika
 
Baraza la mitihani la Taifa(NECTA) limefanya mabadiliko kwenye mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kwa kuondoa machaguo ya majibu kwenye somo la hisabati kuanzia mitihani ya mwaka huu.
Pia wanatarajia kufanya mabadiliko kama haya kwa ngazi ya sekondari kwenye masomo ya fizikia, kiingereza na baiolojia.
Dah hii ishu ya multiple choices kwenye hisabati ilikuwa inaniboa sana!
Weka chanzo cha habari yako.

Ila kama wamefanya mabadiliko hayo wamefanya vizuri.
Hesabu inahitaji kukokotolewa sio multiple choice.

Multiple choice waliwekewe vilaza wa hesabu, sisi mabingwa wa kukokotoa ilikuwa inatutia kichefuchefu.

Namkubali sana Waziri wa Elimu wa sasa Prof. Mkenda, tunamuomba Mama amuache hapohapo miaka 10 asiondolewe.
 
Wanafunzi wa siku hizi hawana uwezo wa kukokotoa mahesabu, itabidi walimu wafundishe kwa bidii mada zote kikamilifu na warudierudie mazoezi mengi kwa wanafunzi. Walimu wote wanaofundisha hisabati wachunguzwa vizuri kama wanamudu vema somo hilo, kwani wengine ni wababaishaji na huruka mada ngumu hawafundishi. Mwalimu aliyesomea arts anawezaje kukokotoa aljebra na jometri? Kuna mambo ya equation, make the subject, find the value of x. Umeenda sekondari ukaishia kusoma arts halafu msingi unang'ang'ana kufundisha hisabati darasa la tatu, nne, la tano unakimbia unapoona mada zinazidi kuwa ngumu. Anajitokeza mwenzako aliyepata F ya math eti naye unamkuta anafundisha la saba anababaisha wananafunzi!
 
Weka chanzo cha habari yako.

Ila kama wamefanya mabadiliko hayo wamefanya vizuri.
Hesabu inahitaji kukokotolewa sio multiple choice.

Multiple choice waliwekewe vilaza wa hesabu, sisi mabingwa wa kukokotoa ilikuwa inatutia kichefuchefu.

Namkubali sana Waziri wa Elimu wa sasa Prof. Mkenda, tunamuomba Mama amuache hapohapo miaka 10 asiondolewe.
Soon nitaweka
 
Kama ya kuchagua jibu sahihi hawawezi je kukotoa wataweza? Watoto watafeli vibaya itabidi standardize ihusike kuinua maksi vingenevyo spoon feeding itatumika
Kuchagua ni ufala sana. Tuliwahi kupewa multiple choices. Jamaa mmoja akaotea maswali yote 10.....tulipomfuata atuelezee hakuna hata kimoja anachojua. Anasema alikua ana guess tu.
 
Wizara ya elimu inaongozwa na vilaza mno. Kila siku wana mapya mara kuweka, kutoa, kubadili, yaani ovyo tu.
 
Yes maana tunahitaji hisabati ya kutenda, tembelea hapa na upige kura yako.

Back
Top Bottom