Nawapongeza Diamond na Harmonize wameonesha weledi na ukomavu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Nadhani kuna siri kati ya wawili hawa... Diamond na Harmonize... Lakini hata kama ni siri lakini wameonesha ukomavu mkubwa kwenye mahojiano yao na media za bongo
Media za kimbeambea na chonganishi sasa inabidi zijipange kweli linapokuja suala la kiwahoji hawa vijana wawili.... Ona majibu ya Diamond

Diamond pia alizungumzia kuhusu Harmonize ambaye ametangaza kujiondoa kampuni ya WCB, “Nimempush Harmonize kufika hapo alipo, nafikiri sasa ni wakati sahihi wengine kuwasapoti, tamanio letu ni kuona tunafanikiwa, naomba watu wamsapoti lengo letu ni kusapoti vijana.”

Jana katika mahojiano hayo Diamond amesema, “nilibahatika kuona post kama watu wengine, na sikujua alilenga kitu gani, lakini Alikiba ni kaka yangu amenizidi umri alianza muziki kabla yangu.”

“Kwenye muziki kuna mambo ya ukitoa wimbo ni kama Simba na Yanga (timu za soka zenye upinzani nchini Tanzania) lakini haiwezi kutia chuki kati yangu na yeye,” amesema Diamond.

Hivi karibuni Harmonize pia alijohiwa na clouds.. Na ni wazi alichomekewa maswali mengi ya wazi na ya mtego ili amkandie Diamond.... Lakini kamwe hakufanya hivyo... Mwishowe aibu ikarudi kwa waandishi...

Hawa waandishi wetu ni lazima watambue kuwa zama zimebadilika. Hizi si zama za akina Hadija Kopa na Nasma Khamisi au Zay B na Sister P. Bifu mpaka mitaani na matusi ya nguoni juu.

Bado kuna shida kidogo kwa Alikiba lakini yeye kwasasa sio habaro tena. Media za bongo sana ni Mondi na Konde boy. Nao wamejua na kujitambua nini kilichopo mbele yao. Wote wanaojaribu kuwachonganisha ni kapuku wasio na mbele wala nyuma.

Ni funzo zuri toka kwa watoto
 
Safi sana wote Mondi na Konde boy ni pro Magufuli.
Mungu awabariki sana Mondi na Konde kwa kuwa upande wa Raisi Magufuli!
 
Bifu ndo hukuza biashara ya muziki popote duniani,na ili bifu itokee lazma kuwepo na uchonganishi ambao ndo sababu ya kuzaliwa au kuendeleza bifu..lkn ktk bifu kila pande inatakiwa kujipanga vilivyo ili mmoja wao asiweze kupotezwa kimbinu na mpnzan wake..akitokea mmoja kashinda bas huyo lazma atafute bifu na mtu wa level yake kwa wakati huo..hii ipo ktk soko la muziki mahali pengi dunian

Bifu hukuza muziki,bifu hukuza biashara pia,bila bifu huwezi jua diamond angekuwa wap leo,alikubali bifu na kuhamishia ktk biashara,amefanikiwa kwa kias kikubwa sasa anarudi na mbinu nyingne..so acha bifu zitafutwe na ziendelee kuwepo
 
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji87][emoji87][emoji87][emoji87][emoji13][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Alikiba ni sawa na Mshana huku jf mambo yake ni ulozi tu mwanzo mwisho
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji116][emoji116][emoji116]
Kwel "uwezo wa kufikiri unatofautiana kulingana na mahitaji"...mtihan mwema mkuu[emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…