Nawasanua wasakatonge wenzangu wenye lengo la kumiliki bajaj, guta au pikipiki na pesa uliyonayo haitoshi kuingia shop

monotheist

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
830
Reaction score
1,449
Wapambanaji wenzangu wenye lengo la kumiliki bajaj, guta au pikipiki na pesa uliyonayo haitoshi kupata chombo kipya ngoja nikusanue labda unaweza kupata muongozo uanzie wapi

1. Kuna bank kama CRDB na MAENDELEO BANK wanatoa bajaj zenye rejesho nafuu kwa msaka tonge ila shida ipo kwenye vigezo vya mkopo vijana wengi wanashindwa kwani BANK wanahitaji mali isiyohamishika na kianzio cha 3m. Ila mkopo wa BANK ni mzuri zaidi kwani lejesho lao kwa siku ni 14k hadi 17k inategemea na aina ya bajaj (mafuta au gesi)

2. SHIRIKISHO hii taasisi inasimama kama mdhamini kwa yule anayetaka kukopa bajaj, pikipiki au guta bank na hana mali isiyohamishika wala 3m pia hana kupitia SHIRIKISHO anaweza kupata kwa kianzio kidogo na rejesho nafuu mfano; bajaj ya mafuta kianzio 2m rejesho per day 17k

3. WATU CREDIT hii taasisi ipo maeneo mengi hapa jijini Dar na inatoa bajaj na pikipiki sina uhakika kama guta pia wanatoa kwa bajaj kianzio ni 1m na rejesho per day 25k

4. MO FINANCE hii ni taasisi ya khanjibai maarufu hapa jiji na ofisi yao ipo katikati mwa jiji la Dar wanatoa bajaj za RE kianzio ni 700k na rejesho per day 28k

Vianzio pamoja na rejesho huwa vinabadilika kutokana na ongezeko la thamani ya chombo husika kwa wakati huo na pia mkataba huwa ni miaka miwili na kama unauwezo wa kupambana chini ya miaka miwili unaongea nao.
 
Kuna mwaka nilikua Korogwe pale Manundu nikakuta NMB wanahimiza watu waende kuchukua bajaji, boda na hizo toyo kwa mkopo.
 
Vipi hali ya UBA na BOLT kwa saivi, kuna maslahi....
 
😂😂😂😂😂 haya mambo ukiwa kichwani haupo vzr unaweza sems utapeli
 
Wapambanaji wenzangu wenye lengo la kumiliki bajaj, guta au pikipiki na pesa uliyonayo haitoshi kupata chombo kipya ngoja nikusanue labda unaweza kupata muongozo uanzie wapi

1. Kuna bank kama CRDB na MAENDELEO BANK wanatoa bajaj zenye rejesho nafuu kwa msaka tonge ila shida ipo kwenye vigezo vya mkopo vijana wengi wanashindwa kwani BANK wanahitaji mali isiyohamishika na kianzio cha 3m. Ila mkopo wa BANK ni mzuri zaidi kwani lejesho lao kwa siku ni 14k hadi 17k inategemea na aina ya bajaj (mafuta au gesi)

2. SHIRIKISHO hii taasisi inasimama kama mdhamini kwa yule anayetaka kukopa bajaj, pikipiki au guta bank na hana mali isiyohamishika wala 3m pia hana kupitia SHIRIKISHO anaweza kupata kwa kianzio kidogo na rejesho nafuu mfano; bajaj ya mafuta kianzio 2m rejesho per day 17k

3. WATU CREDIT hii taasisi ipo maeneo mengi hapa jijini Dar na inatoa bajaj na pikipiki sina uhakika kama guta pia wanatoa kwa bajaj kianzio ni 1m na rejesho per day 25k

4. MO FINANCE hii ni taasisi ya khanjibai maarufu hapa jiji na ofisi yao ipo katikati mwa jiji la Dar wanatoa bajaj za RE kianzio ni 700k na rejesho per day 28k

Vianzio pamoja na rejesho huwa vinabadilika kutokana na ongezeko la thamani ya chombo husika kwa wakati huo na pia mkataba huwa ni miaka miwili na kama unauwezo wa kupambana chini ya miaka miwili unaongea nao.
Vp kwa sisi ambao tuko mikoani tunawezaje kupata huduma hizi
 
Back
Top Bottom