Nawashangaa vijana wa Kenya, hakuna nchi itakayoweza kuendeshwa bila kodi

gstar

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
790
Reaction score
1,373
Wakati nikiutafakari umasikini wa Mwafrika na vipi tutajikwamua kutoka hapa tulipo nakutana na mauzauza ya wananchi wakenya wanao andamana kisa ongezeko la kodi katika bidhaa mbalimbali. Nimekaa nikajiuliza ikiwa sisi waafrika tunataka kujitegemea kiuchumi, nivipi tutaweza kuziepuka hizi kodi katika bidhaa mbali mbali.

Katika mawazo yangu nimegundua kwamba kodi ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa, leo hii ukiangalia bajeti zetu zilizopitishwa na mabunge ya Afrika Mashariki kwa pamoja utagundua kwamba asilimia kubwa tunategemea wafadhili ama mikopo ili tuweze kupata fedha za kuendesha nchi zetu na kulipa mishahara pamoja na miradi ya maendeleo. Si ajabu kuona madeni ya nje yakikuwa na kuongezeka kwa kasi ya ajabu na tusilalamike maana ndivyo tunavyo taka.

Swali la kujiuliza, Je ni lini mataifa ya Afrika hususani Afrika Mashariki yataweza kuondokana na utegemezi huu wa kiuchumi? Jibu ni pale ambapo tutatoza kodi stahiki kwa kila bidhaa, tutazitumia kodi hizo kutekeleza malengo mahususi yaliyo kubaliwa na pia tutapunguza ufisadi na rushwa ili kodi zinazo kusanywa ziende kutenda mambo yaliyo kusudiwa.

Ni kwanini wananchi wanaandamana kupinga miswada ya kodi kila inapo pelekwa bungeni? Jibu ni moja tu, hatujazoea kujitegemea kama Waafrika, hatuaminiani pia kwani tumejifunza kutoka kwa watangulizi wetu walio kusanya mapato na kuvimbisha matumbo yao na ya familia zao, ama tunaishi kwenye lindi la umasikini kiasi kwamba kile kidogo tunacho kipata tunadhani si haki yetu kutozwa kodi maana ni kama kumuomba maiti damu!

Serikali za mataifa ya Afrika haswa Tanzania wajifunze kutoka kwenye maandamano ya Wakenya kwani si kwamba Watanzania hawana manung'uniko hayo, la hasha! Manung'uniko hayo yapo ila tu ni kwamba wameshindwa kupata pa kuyapeleka wamebaki wakilalama kwenye mabaa ama kwenye vijiwe vya kahawa huku wakitazamana usoni isije kuwa kuna shushushu mmoja katumwa kuwarekodi na kisha awapeleke sehemu stahiki, kiufupi tunaishi kwa mashaka.

Vijana wa Kenya waache kufuata mkumbo, watambue kuwa malipo ya kodi hayaepukiki ili tuweze kuendelea na kujitegemea kama Waafrika, tunapaswa kulipa kodi. Hata hao wazungu wanao tuchangia mamilioni ya Madola na Mapaundi na Mayuro, wanalipishwa kodi kikamilifu na serikali zao. Kwa nchi zilizo endelea ni kosa la jinai linalopelekea hata kifungo cha maisha ama kunyongwa pindi raia atakapo kamatwa akiwa amejaribu kukwepa kodi kwa njia moja ama nyingine.

Kwa Afrika swala la kukwepa kodi halali ni swa ambalo linasemwa na kulalamikiwa na watu wengi. Rushwa inachangia kupoteza pesa zilizo halali kulipwa kwa njia ya kodi. Kama tunataka kuimarisha uchumi wa mataifa yetu basi hatuna budi kulipa kodi stahiki na serikali zetu zisimamie ipasavyo masuala yote ya malipo ya kodi. Asipatikane bwenyenye yoyote atakaye pendelewa ama kukandamizwa kwenye hili, maswala ya kodi tuyachukulie kwa uzito wake.

Kwaleo sina mengi niwapongeze Wakenya kwa kuonyesha ukomavu wa kidemokrasia lakini isije ikawa ule usemi wa, "Ukimsifu mgema tembo huitia maji!"

Wakatabahu.
 
Unashangaa kwa sababu akili yako ndogo
 
Wewe ni mfano tu, mko mamilioni wenye mawazo ya hivyo. Hakuna mtu anayekataa kulipa kodi. Je hizo kodi zinatumiwa ipasavyo? Kenya kuna ufisadi wa laana na bado wanakopa sana. Achana na watu wa Kenya, wanajaribu kutatua matatizo yao.

Deal na nchi yako, hapa tuna matatizo, zaidi ya wakenya ila tunayaacha yapite kama hatuoni na hatusikii. Ule mwenge ukiachwa, huenda akili zitawarudi.
#Nasimama na vijana wa Kenya
 
Wakati nikiutafakari umasikini wa Mwafrika na vipi tutajikwamua kutoka hapa tulipo nakutana na mauzauza ya wananchi wakenya wanao andamana kisa ongezeko la kodi katika bidhaa mbalimbali. Nimekaa nikajiuliza ikiwa sisi waafrika tunataka kujitegemea kiuchumi, nivipi tutaweza kuziepuka hizi kodi katika bidhaa mbali mbali.

Katika mawazo yangu nimegundua kwamba kodi ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa, leo hii ukiangalia bajeti zetu zilizopitishwa na mabunge ya Afrika Mashariki kwa pamoja utagundua kwamba asilimia kubwa tunategemea wafadhili ama mikopo ili tuweze kupata fedha za kuendesha nchi zetu na kulipa mishahara pamoja na miradi ya maendeleo. Si ajabu kuona madeni ya nje yakikuwa na kuongezeka kwa kasi ya ajabu na tusilalamike maana ndivyo tunavyo taka.

Swali la kujiuliza, Je ni lini mataifa ya Afrika hususani Afrika Mashariki yataweza kuondokana na utegemezi huu wa kiuchumi? Jibu ni pale ambapo tutatoza kodi stahiki kwa kila bidhaa, tutazitumia kodi hizo kutekeleza malengo mahususi yaliyo kubaliwa na pia tutapunguza ufisadi na rushwa ili kodi zinazo kusanywa ziende kutenda mambo yaliyo kusudiwa.

Ni kwanini wananchi wanaandamana kupinga miswada ya kodi kila inapo pelekwa bungeni? Jibu ni moja tu, hatujazoea kujitegemea kama Waafrika, hatuaminiani pia kwani tumejifunza kutoka kwa watangulizi wetu walio kusanya mapato na kuvimbisha matumbo yao na ya familia zao, ama tunaishi kwenye lindi la umasikini kiasi kwamba kile kidogo tunacho kipata tunadhani si haki yetu kutozwa kodi maana ni kama kumuomba maiti damu!

Serikali za mataifa ya Afrika haswa Tanzania wajifunze kutoka kwenye maandamano ya Wakenya kwani si kwamba Watanzania hawana manung'uniko hayo, la hasha! Manung'uniko hayo yapo ila tu ni kwamba wameshindwa kupata pa kuyapeleka wamebaki wakilalama kwenye mabaa ama kwenye vijiwe vya kahawa huku wakitazamana usoni isije kuwa kuna shushushu mmoja katumwa kuwarekodi na kisha awapeleke sehemu stahiki, kiufupi tunaishi kwa mashaka.

Vijana wa Kenya waache kufuata mkumbo, watambue kuwa malipo ya kodi hayaepukiki ili tuweze kuendelea na kujitegemea kama Waafrika, tunapaswa kulipa kodi. Hata hao wazungu wanao tuchangia mamilioni ya Madola na Mapaundi na Mayuro, wanalipishwa kodi kikamilifu na serikali zao. Kwa nchi zilizo endelea ni kosa la jinai linalopelekea hata kifungo cha maisha ama kunyongwa pindi raia atakapo kamatwa akiwa amejaribu kukwepa kodi kwa njia moja ama nyingine.

Kwa Afrika swala la kukwepa kodi halali ni swa ambalo linasemwa na kulalamikiwa na watu wengi. Rushwa inachangia kupoteza pesa zilizo halali kulipwa kwa njia ya kodi. Kama tunataka kuimarisha uchumi wa mataifa yetu basi hatuna budi kulipa kodi stahiki na serikali zetu zisimamie ipasavyo masuala yote ya malipo ya kodi. Asipatikane bwenyenye yoyote atakaye pendelewa ama kukandamizwa kwenye hili, maswala ya kodi tuyachukulie kwa uzito wake.

Kwaleo sina mengi niwapongeze Wakenya kwa kuonyesha ukomavu wa kidemokrasia lakini isije ikawa ule usemi wa, "Ukimsifu mgema tembo huitia maji!"

Wakatabahu.
 
Na wao watakushangaa wewe kwa kutowaelewa, hawajasema hawataki kulipa kodi, maana tayari wanalipa, wanachopinga ni ongezeko la kodi ambalo linawaongezea umasikini zaidi.
 
Back
Top Bottom