Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Kazi ya kwanza ya serikali ni kulinda uhai wa wananchi. Pili ni kulinda mali zao. Ibara ya 14 ya katiba ambayo ndiyo sheria mama inasema "kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria."
Ni kwa mujibu wa sheria tu uhai wa mtanzania unaweza kuondolewa mfano kama atakutwa na hatia inayostahiki anyongwe, akiuawa wakati anamshambulia mtu, akifa vitani, na akiuawa na mtu mwingine au wengine ambao lazima washitakiwe.
Na adhabu ya kuondoa uhai ni kifo kwa mujibu wa sheria ya jinai chini ya kipengele cha 197 cha Kanuni ya adhabu. Zaidi ya hapo, awe mtu au mamlaka inayotoa uhai wa mtanzania kwa kutenda au kutotenda, inapaswa kushitakiwa.
Hivyo, kwa msingi huu, nashauri wahanga wa Kariakoo waishitaki Jamuhuri pamoja na mwenye nyumba kwa uzembe au omission na kutenda kinyume commission ili watiwe adabu nao wapate haki yao hata kama uhai wao hautarudishwa.
Wapo walioacha mayatima, wajane, wazazi wazee na wengine waliokuwa wakiwategemea.
Nawasilisha.