Nawashtaki kwa Imamu.

Nawashtaki kwa Imamu.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
NASHTAKI KWA IMAMU.


1)Kwa mnayonifanyia,roho yangu inauma

Imamu nitamwambia,aje wakanya mapema

Wapo nilowasikia,jinsi wanavyonisema

Ramadhani Ramadhani,ndo mwezi wangu wa swala.




2)Imamu nakuambia,Mimi ni mtu mzima

Vidole Waninyoshea,hawanisemi kwa mema

Siyo wananiusia,Bali wananisakama

Eti Mimi muumini,naabudu Ramadhani.



3)Masijidi naingia,kumuabudu karima

Vipi wananikandia,kwa yalotokea nyuma

Bwana imamu sikia,vipi nanze mpya zama

Ramadhani ikipita,nisondoke masijidi ?.



4)Vidole waninyoshea,wakitaka nisukuma

Eti wanajisemea,sikuwa siku za nyuma

Hovyo ninajifanyia,Mimi ni mtu si duma

Kama nilijisahau,mbona mkuniusia ?


5)Kusemana nachukia,huu mwezi wa rehema

Masijidi naji jia,nami nipate Neema

Hasira sijepatia,ndio mana najituma

Imamu kawaambie,sitaki kusemwa semwa.


SHAIRI- NASHTAKI KWA IMAMU.

MTUNZI-Idd Ninga,Arusha.

+255624010160

iddyallyninga@gmail.com
 
Ramadhan ya ramadhan ya musima lqur an akhbarta bilbushra alkhayr walghufran ramadhan anwarun yajaa ika liman
Ulikua ni utenz tulifundishwa madrasa enzi hizo ulitoka katika moja ya vitabu vya lugha kuuhusu huu mwezi mtukufu
 
Back
Top Bottom