Natanguliza shukrani zangu kwa mwenyezi mungu kwa kila jambo alilolitenda kwangu.lakini nitakuwa mkosefu wa fadhila kama sitowashukuru kaka na dada zangu wa hapa jf kwa ushauri walioutoa nilipotoa ombi langu la ushauri kwao.hakuna aliyesita kutoa ushauri ukiachilia mbali wale wanaochukulia mambo kirahisi.kimsingi baadhi ya ushauri mlionipa hasa kwenye pm umezaa matunda.hivyo nafikiri wale wote waliotoa ushauri kwamba nisiolewe walikuwa kwenye upande wa mungu muweza wa yote.mungu awabariki na jumapili njema.