Nawatakia heri CCM katika Mkutano wao Dodoma

Nawatakia heri CCM katika Mkutano wao Dodoma

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Hapa nataka kuandika something like an imaginary speech kuwaalika wajumbe. Kama anavyofanya Xi Jin Ping. Wengine labda watataka kuiendeleza.

Karibuni Dodoma wajumbe wote. Tunakutana katika hali ambapo changamoto nyingi zinatukabili, kwa mfano vita ya Ukraine ambayo inayumbisha uchumi wa Dunia, na matatizo ya tabia nchi.

Kazi kubwa inatukabili katika kuwaongoza wananchi katika kipindi hiki kigumu, lakini tukiwa na umoja na ushirikiano, tukiwa na lengo moja, tukiwa na juhudi, tukiwa na imani, na tukizingatia mambo mema yaliyofanywa na watangulizi wetu, waasisi wa Chama chetu ambacho awali kiliundwa kugombea Uhuru lakini sasa kinapigania maendeleo ya watu: tutashinda.

Tunakabiliwa na matatizo ya Ulinzi na usalams katika Jumuia ya Africa Mashariki: tukiishi kwa umojs, tutaweza kuyakabili haya matatizo. Kila mtu lazima atoe mchango wake ili aweze kuendeleza taifa. Tuzingatie afya, Taifa litajengwa na watu wenye afya, kwa hiyo tabia zozote ambazo zina athari mbaya kwa afya mwanaCCM hapaswi kuwa nazo. Ni tabia tabia ambazo zitakwamisha mapinduzi ya kisiasa na kijamii tunayotaka kufanya..

Tuzingatie maadili: mambo mengi yanadaiwa kuwa maadili mema ambayo hayana maana sana, lakini yapo mambo ya msingi ya maadili yakikiukwa, tunawadhuru wengine na pia tunajidhuru nafsi zetu. King Charles III aliwahi kusema hapo zamani, kwamba "some things we ignore at our own peril" . Kwamba tunajidhuru wenyewe tukiyapuuzia mambo mengine.

Nawatakia heri katika huu mkutano. Kuchekecha majina 2000 ni kazi kubwa; kuamua huyu baradhuli, hafai, huyu elimu yake haitoshi, huyu hana uzoefu, hana experience,huyu hivi, huyu vile.
 
Back
Top Bottom