Nawatakia kheri kidato cha nne, 2014

karim kid

Member
Joined
Oct 7, 2014
Posts
19
Reaction score
3
Kwa wale wadogo zangu wanao tarajia kuanza mitihani yao ya taifa hivi karibuni,ningependa kuitumia hii fursa kuwatakia mitihani myema..Tupo pamoja katika kuwaombea na nnaimani matokeo yatakuwa mazuri..
Kikubwa ni kujiamini na kuhakikisha unafaya maswali yote uliyo chagua..mtahiniwa asiwe na presha ya mtihani kwasababu maswali yatakayo ulizwa yanatoka kwanye mtaala au SYLLABUS..
FUATA MAELEKEZO KWA USAHIHI wakati unajibu mtihani wako na usitumie muda mwingi sana kwenye swali moja.Natumai huu ndio mchango wangu mkubwa kwa hawa wasomi wetu..lazaidi sina ila tu nazidi kuwaombea kwa Mungu mambo yatakua mazuri..:A S 11:

CHANZO: NIPASHE
 
Kesho ndio siku ya kipimo cha mwisho cha ulichokipanda takribani kwa miaka minne. binafsi nilifanya mtihani wangu mwaka 2007. Fanyeni vizuri hatutaki mkifeli msingizie eti FB,JF NA WHATSAP SIJUI NDIO ZIMESABABISHA.

Mungu Awabariki na Awalinde.
 
Duuh! mwaga lutila, F4 2007? kakojoe ukalale.

Mbona mimi naona ni mda sana kaka, hapa nilipo ni baba wa watoto 4. Nenda kule kwenye jukwaa la MMU, CHIT CHAT NA CELEBRITIES usishangae kuna watoto wa FORM 3 KAKA.
 
Hiyo title kidogo imeniacha hoi ingawa nimeelewa ulitaka kusema nini!
 
Wafuate Facebook watakie mtihani mwema, wapo kule na hata kesho utawakuta. Humu labda kuna ma QT japo wanajielewa ni mwezi sasa wame log off
 
Kesho ndio siku ya kipimo cha mwisho cha ulichokipanda takribani kwa miaka minne. binafsi nilifanya mtihani wangu mwaka 2007. Fanyeni vizuri hatutaki mkifeli msingizie eti FB,JF NA WHATSAP SIJUI NDIO ZIMESABABISHA.

Mungu Awabariki na Awalinde.

Magoli yamepanuliwa, BRN inafanya kazi kila mmoja atafaulu. ndio maana mwaka huu form six almost wote wamefaulu hata PCB ambayo huwa inaletaga tabu majority wana B na B+ na C pass ambazo zilikuwa dimu huko nyuma!
 
Mbona mimi naona ni mda sana kaka, hapa nilipo ni baba wa watoto 4. Nenda kule kwenye jukwaa la MMU, CHIT CHAT NA CELEBRITIES usishangae kuna watoto wa FORM 3 KAKA.

Mkuu umefanya vizuri sana kuwakumbuka wadogo zetu na kuendelea kuwaombea ili wasichore mazombie na kuandika mistari ya Diamond.
 
Wafuate Facebook watakie mtihani mwema, wapo kule na hata kesho utawakuta. Humu labda kuna ma QT japo wanajielewa ni mwezi sasa wame log off

Hapana si wote wako Fb wengine tuko huku.

Tunashukuru sana kwa best wishes zako mtoa mada..
 
Mungu awatangulie ktk mtihan wao
 
Mungu awatangulie ktk mtihan wao

best wishes to all form IVs... ndo paper lenye presha ya kufaulu sana yani ..advance ni presha ya kukimbizia boom na chuo kizuri kama ud ..muhas ARU.. japo kanaitaji umakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…