Nawatakia kheri kidato cha nne, 2014

Toa neno lolote hapa kuwatakia kheri ya baraka wadogo kwa wakubwa zetu wanaotarajia kuanza mtihani wao wa kuhitimu kidato cha nne NOVEMBER 2014.
 
Wanafunzi munaoenda kufanya mtihani kesho,zingatieni yafuatayo,1.maelekesho ya msimamizi,2,soma kwa makini maswali iliuelewe kuwa linahitaji nini?.3.usihofu au kuogopa[jiamini].na sisi tunawatakia mtihani mwema na mungu awatangulie amina.
 
Tutapata ma barmaid wa kutosha na wanenguaji wa kutosha.
 
Tunawaombea watulie wafanye vema katika mitihani yao, wasidanganyike wakirudi mtaani maisha hayana shortcut na elimu pekee ndio mkombozi wao na urithi bora
 


Napenda kuchukua fursa hii kuwatakia kila la kheri wanafunzi wote wa kidato cha nne wanaotarajia kuanza mitihani yao ya kitaifa leo tarehe 03/11/2014. Ni ukweli usiopingika kwamba wanafunzi hawa wamepitia hatua ndefu yenye vikwazo anuai hadi hatua hii waliyofika. Kumbuka kwamba kuna wenzao wameishia njiani kwa kushindwa kuruka viunzi hivi na hivyo kujikuta wakikatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutundikwa mimba (kwa sababu ya viherehere vyao – by Profesa JK ), kukosa karo, umbali mrefu wa shule, utovu wa nidhamu, kuvuta bangi, n.k.



Lakini pia, naomba kuchukua nafasi hii kuwapa pole wanafunzi wa Shule za Kata wanaosoma ktk shule ambazo hazina madarasa, maabara, walimu, vitabu, maktaba, chakula, mazingira rafiki, n.k. Hili kundi linapaswa kuonewa huruma kwa kuwa serikali yetu tukufu imeamua kwa makusudi kabisa kuwatelekeza watoto hawa na kuwakosesha fursa ya kuelimika.



Wakati mamia ya watoto wa masikini wakisomea chini ya miembe, mikorosho na mibuyu, watoto wa MAFISADI, WASAKATONGE NA WACHUMIA TUMBO wachache wanapata elimu yao katika shule zenye ubora wa kutosha na ambazo zimesheheni walimu wazuri, maabara, vitabu, maktaba, mazingira rafiki ya kujifunzia na kila aina ya rasilimali zinazowawezesha kupata elimu bora.



Lakini pia nitoe pole kwa wale watoto wa mafisadi waliozoea kusoma kwa ulegevu huku wakitegemea kupata matokeo bora. Hili ni kundi la wanafunzi wanaojihusisha na kila aina ya USHENZY shuleni…ikiwamo kufanya umalaya, kutozingatia masomo ipasavyo, kufanya mzaha kwenye masomo na kushinda kwenye mitandao ya FESIBUKU, TWITA na WASAPU wakitafuta wanaume wa kuwadinya! Mimi nasema kwamba hawa wanafunzi wafeli tu kwani hawana adabu. Badala ya kuzingatia masomo, wao wameelekeza akili zao kufanya UPUMBAVU! Wafeli tu, maana hakuna namna nyingine….tumechoka! Sitegemei kuwa adui kwa sababu ya kusema ukweli….nimeweka picha ili kuonyesha ushahidi wa kile ninachokisema.

View attachment 198593 View attachment 198597

Wanfunzi hawa wamefikia hatua ya kubuni mbinu mbalimbali za kuigilizia ili wafaulu, pamoja kwamba wazazi wao wanawasomesha kwenye shule nzuri. Mimi nasema kwamba wafunzi wa aina hii, hakuna haja ya kuwaonea kuruma…wafeli tu ili liwe fundisho kwa wazembe wengine…tumechoka kuona watoto wa wakulima wakisomeshwa kwenye shule ambazo hazina walimu wakati watoto wa mafisadi wanasoma shule za maana lakini wakitegemea ubwete!



Hii ni aina ya wanafunzi ambao wakiingia kwenye chumba cha mtinani huandika utumbo! Badala ya mwanafunzi ku-balance entries kwenye Trial Balance, yeye ama huchora nyumba, Zombie au kuandika ujinga mwingine wanaoujua wenyewe! Hawa nao wafeli tu kwani inaonekana hawajui wameenda shule kufanya nini!




:yield:
 
Tutapata ma barmaid wa kutosha na wanenguaji wa kutosha.

Mtu mzima inatakiwa kuwa na busara kwenye vitu vya maana sio unakurupuka kutoka chooni halafu unacomment, utacomment upuuzi kama ulioufanya, watoto wako ndio watakuwa barmaid na wacheza shoo, mungu awabariki wote mnaofanya mitihani ya kidato cha 4, mungu awabariki muanze salama mmalize salama,amen.
 
peleka mshono huko mmasai mchambia rungu,kavae chupi kwanza,nyie si hamvaagi chupi?
 
Tunawatakia mtihani mwema form four wote, bila kumsahau shemeji yangu Heriette. Namuombea sana kwa mungu afauulu mtihani wake wa form four vizuri
 
Tunawatakia mtihani mwema form four wote, bila kumsahau shemeji yangu Heriette. Namuombea sana kwa mungu afauulu mtihani wake wa form four vizuri

Yeah Heriete ashakua mtu mzima sasa mumuache kidogo apumue sawa??
 
Eee Mungu wasaidie na uwajalie afya njema kwa muda wote wa mitihani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…