Mary Chuwa
Senior Member
- Feb 24, 2011
- 177
- 40
Kipindi cha Kwaresima kinakaribia kufika ukingoni.
Nawatakia maandalizi mema ya Pasaka,Yesu anapofufuka,akafufuke katika uchumi wa familia zenu,mahusiano mema ya familia zenu,na Upendo uliokwisha poa na kufa nao ukawe na Uhai Mpya.
Afya njema katika familia zenu
Pasaka hii watu muwe karibu na familia na jamaa zenu na siyo kuitumia kuwasaliti wengine.
yale mema mliyokuwa mnayafanya wakati wa Kwaresima basi yakawe Mwendelezo katika maisha Yenu.
Kila la kheri Wapendwa katika Maandalizi ya Ufufuko wa Yesu

Usitutie katika vishawishi lakini utuokoe maovuni. Amina. Mary uwe na Pasaka njema na weweSawa Fidel80,funga macho na ufuatishe sala hii,
Baba Yetu Uliye Mbinguni
Jina Lako Litukuzwe
Ufalme Wako Ufike
Utakalo Lifanyike
Duniani Kama Mbinguni
Utupe Leo Mkate Wetu wa Kila Siku
Utusamehe Makosa Yetu
Kama Tunavyowasamehe na sisi waliotukosea...........................
Samahani Fidel80 fungua macho kwanza hapa unapoomba msamaha kwa Mungu hakikisha umewasamehe kweli waliokukosea
Haya tuanze tena
Usitutie katika vishawishi lakini utuokoe maovuni. Amina. Mary uwe na Pasaka njema na wewe