Nawatakia Sikukuu Njema Ma-House Girl na Ma-House Boy

Nawatakia Sikukuu Njema Ma-House Girl na Ma-House Boy

Obuntu

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2008
Posts
510
Reaction score
34
Napenda nichukue nafasi hii kuwatakia Sikukuu njema wafanyakazi wote wa majumbani. Pia natumia fursa hii kuwashukuru kwa kazi kubwa wanazofanya majumba, kwa maana bila wao familia zetu nyingi zingekuwa mashakani.

Najua siku ya kesho mtakuwa na kazi nyingi sana hasa hasa zinazohusiana na kupika na usafi wa nyumba kwa ujumla. Jaribu kutumia wakati huo kuongea na ma-boss wenu kama kuna kitu kinawatatiza maana ma-boss wote kesho watakuwa nyumbani na watakuwa wanafuraha sana, ukizingatia pia mapochi yao yatakuwa na maela ya kutosha.

Pia nawaombeni ma-boss kuwanunulia zawadi hawa wasaidizi wetu maana wao ndiyo wanaijua vizuri nyumba kuliko hata sisi! Wapeni shukrani kwa kuwalelea watoto na usaidizi mwingineo.

Asanteni Sana na Mungu awabariki..
 
Hawaruhusiwi kuingia JeiEff.....nani atawafikishia ujumbe???
 
duuuh!kweli lile ni kundi maalumu katika jamii.
 
hivi watakuwa na wao wanasoma JF eeeh?
 
Hawaruhusiwi kuingia JeiEff.....nani atawafikishia ujumbe???

Wanaruhusiwa - Jamii Forum!

Ukifika nyumbani waambie kuwa TUNAWAPENDA na TUNATHAMINI UWEPO WAO!
 
Back
Top Bottom