Nawaza ila ni ndoto

Nawaza ila ni ndoto

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Nawaza sana ile siku ya tarehe 17/03/2020 tulipoondokewa na Rais wa jamhuri ya Tanzania ni siku ambayo nilifikiria mengi kuhusu siri ya ulimwengu na jinsi unavyojiendesha(endeshwa),ila niliishia kwa kusema sifa kuu apewe muumba wa mbingu na ardhi yake ni yeye mwenye kuunda na kuboa hivyo sikushangaa sana kuhusu kifo kwani tulishawazika wengi sana sana..nilimkumbuka marehemu babu yangu kwa huzuni mkubwa.

Kwa masikitiko makubwa nilichukua simu yangu na kufungua data ghafla notification ya jamii forums ikaingia kunijulisha habari hiyo,leo nimepumzika zangu home nimejikuta nafatilia miradi yote iliyoanzishwa na hayati Rais John Magufuli ikiwemo
i.Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115).
ii.miradi ya barabara
iii.reli ya kisasa
iv.sakata la machinga
v.ulinzi na usalama
vi.uwajibikaji
vii.vita dhidi ya rushwa
viii.airtanzania

Nimewaza utekelezaji na mikakati iliyosukwa katika kutufikisha nchi ya ahadi,ufatiliaji wa miradi hii na kuiona kua itakufa au haitaisha kwa wakati ukweli nimewaza.mfumo wa ujamaa na falsafa aliyoitaka kuijenga katika nchi itakuja na itaenziwa kwa msingi ipi bado nilitafakari kwa kina.

Punde iliingia notification ya kunijulisha kuwa rubi uzito wa gm 2 imekamatwa na ipo nyengine ya kg 2 imetoroshwa ,serikali haina taarifa ya mirabaa zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari daah ukweli niliwaza.

Ghafla nimeona taarifa za CAG akiongelea ukamilifu la bwawa la ufuaji wa umeme kuwa lipo nyuma kwa asilimia 45 kuwa halijulikani ni lini litakamilika inawezekana ujenzi wake ni wakusuasua.

Kidogo nimezipata taarifa kuwa ile reli haijakamilika kwa wakati sahihi ni 49% na siyo 94%‎ iliyotarajiwa kufikia mwaka huu.sijakaa vizuri nimejikuta napokea taarifa kuwa suluhu anasema kuwa hakuwa comfortable kwenye uongozi ulopita kwani ilikuwa hawakubaliani kwa mambo kadhaa.

Sijakaa vizuri nimesikia Mh Makonda amerudishwa serikalini ndiyo apo ghafla nikashtuka kutoka usingizini na muda wa futari ulishakaribia.
 
Lakini Tanzania bado inasonga mbele, nyie endeleeni kuwaza yaliyopita ila rais ni mama ,
 
Kila mmoja nduniani huwa anapenda kufanya kitu ambacho nafsi yake inakipenda na kuridhika nacho.
 
Back
Top Bottom