Nawaza kuleta Friday talk show

Nawaza kuleta Friday talk show

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Habari wana MMU,

Nitakua naweka mada kila Ijumaa zinazohusu mambo mbalimnali kama wanawake, watoto, mahusiano nk. Lengo la mada hizi ni kutoa elimu kwa jamii.

Mada hizo zitakuwa zinawasilishwa mapema na Mjadala utaanza saa sita mchana.

Mimi ninaomba Moderators watusaidie kuongoza mjadala huu ili kuweka mambo sawa. Kila atakayeshiriki atoe mawazo bila kutoka nje ya mada au kuleta mizaha na utani.

Ijumaa hii (Tarehe 16/4/2021) nitaanza na mada inayohusu 'Unyanyasaji wa kingono kwa watoto (wa kike na wa kiume)'

Asanteni.
 
CRITIC:

Hizo mada si ndio kila siku zinajadiliwa humu?

Huoni kama utaleta thread mrudiano kila siku?

Je ulifikiria kuwa moderators wanaweza kuunganisha au kufuta uzi wako kutokana na kufanana maudhui na mada zilizojadiliwa huko nyuma?

Je, unadhani hao mods wataweza kuongoza mjadala mwanzo mwisho?
 
Kuna mambo mengi kama taifa ya kuongelea. Ngono haijawahi kua tatizo la mtanzania. Bali uhaba wa elimu, maji, miundombinu, siasa, uchumi na mengine mengi.
 
Habari wana MMU,

Nitakua naweka mada kila Ijumaa zinazohusu mambo mbalimnali kama wanawake, watoto, mahusiano nk. Lengo la mada hizi ni kutoa elimu kwa jamii.

Mada hizo zitakuwa zinawasilishwa mapema na Mjadala utaanza saa sita mchana.

Mimi ninaomba Moderators watusaidie kuongoza mjadala huu ili kuweka mambo sawa. Kila atakayeshiriki atoe mawazo bila kutoka nje ya mada au kuleta mizaha na utani.

Ijumaa hii (Tarehe 16/4/2021) nitaanza na mada inayohusu 'Unyanyasaji wa kingono kwa watoto (wa kike na wa kiume)'

Asanteni.
Wala sio lazima kuomba ruhusa. Wewe leta tu mada. Halafu uone response na reaction inakuwaje. Hapo ndio utajifunza kama mada yako ina mvuto au la.
 
CRITIC:

Hizo mada si ndio kila siku zinajadiliwa humu?

huoni kama utaleta thread mrudiano kila siku?

je ulifikiria kuwa moderators wanaweza kuunganisha au kufuta uzi wako kutokana na kufanana maudhui na mada zilizojadiliwa huko nyuma?

Je, unadhani hao mods wataweza kuongoza mjadala mwanzo mwisho?
Ndio maana nimeomba msaada wa usimamizi kutoka kwao, naamini watafanya hivyo kwa kua ndio wajibu wao.

Na ikitokea kuna chochote kimeenda nje ya mada basi nitareport kwao.
 
Wala sio lazima kuomba ruhusa. Ww leta tu mada. Halafu uone response na reaction inakuwaje. Hapo ndio utajifunza kama mada yako ina mvuto au la.
Asante kwa ushauri mkuu.
 
Back
Top Bottom