mangyi
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 723
- 877
Wakuu naamini mu wazima na mnaendelea vizuri na TOZO.
Mimi nimekutana sana na visa vya kupendwa na wake za watu kimasihara sihara mpaka nahisi ni pepo. Wadada single nawapata kwa nadra sana.
Ila kati ya hao wote kuna huyu mmoja ambae alitokea kuzama zaidi.
Huyu binti ni mrembo haswa picha zake hua natamani nizitupie kule kwenye uzi wa WAREMBO WORLD WIDE ila nahisi anafahamika. Huyu mrembo kwa madai yake alitokea kunipenda sana kiukweli na mimi nilimpenda japo tulichelewa kuambiana mpaka yeye kuolewa.
Tatizo ni kwamba wote tuliulizia habari za kila mmoja wetu kwa wrong people. Yeye aliulizia kwa binti mmoja niliyekua na mazoea nae na yule binti akamjibu kwamba nina mchumba ambaye tutaoana. Mimi pia nikaulizia kwa rafiki yake wa kike na majibu yalikua kwamba miezi kadhaa mbele huyu binti ataolewa. ( Hili nilikuja kuligundua kua ni uongo kwa sababu baada ya yeye kuolewa tulizungumza akafunguka ukweli wote kwa uchungu. Yeye alinieleza alivyoambiwa na mimi nilipomueleza nilivyoambiwa alinijibu kuwa aliamua kumkubalia jamaa baada ya kuhisi kuwa hatuwezi kua na mahusiano kwa hali hii.)
Siku tulipoongea aliniambia kuwa, japo ameolewa ila bado anahisia na mimi😋😋. Inafikia wakati inabidi aamke usiku atafute chimbo tuongee video call.
Nakumbuka kipindi anakaribia kufanyiwa Send-off party aliniambia tutoroke nae tuende mbali nikakataa. Alikua tayari kwa lolote kwangu. Ila status ya wazazi wake na mambo ya kikanisa yalisababisha nione nitakua na hatia kufanya hivyo.
Nimewahi kukutana nae cku wanatoka kwenye mafundisho ya ndoa wakiwa na mume wake mtarajiwa (wakati huo). Waliitisha piki piki ili waondoke eneo la kanisani kuelekea nyumbani. Alivyoniona tu akagoma kupanda piki piki moja na mumewe akadai aitiwe yakwake. Alivyofika tu home akanipigia kuniomba msamaha kwa kushindwa kunisalimia pale. Na akaniambia aligoma kupanda piki piki moja na jamaa ili asiniumize (ila mimi siumiagi juu yake)
Kwa sasa wapo kwenye ndoa na ina muda kiasi ila hachoki kunitafuta na kutaka nikale tunda kimasihara. Na mimi nashawishika kwenda kula.
Siombi ushauri kwa sasa ila nasubiri nile tunda, ninogewe na jamaa asanuke, akishasanuka aanze kunitafuta ili aniue. Ndo nitarudi kwenu ndugu zangu kuwaomba ushauri kama jamaa atakua hajaniwahi. Akiniwahi nitamuomba niwape mrejesho kabla sijasepa. Kama atakua hajaniwahi najua mtanishauri. Wakati huo msisahau kukumbuka huu uzi.
Asanteni na mnitake uzinzi mwema. Ila nampenda huyu bint. Wazee wa "picha tafadhali" msiombe picha kwa kua sitawapa.
Niwaage kwa jina la tozonia