Nawaza kwa sauti: Rais akiamua kuzifuta kabisa sherehe za uhuru tutamfanya nini?

Nawaza kwa sauti: Rais akiamua kuzifuta kabisa sherehe za uhuru tutamfanya nini?

G4N

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
4,283
Reaction score
9,925
Ndiyo! Hakuna la kumfanya, kwasabb katiba imesema rais hashitakiwi kwa jambo lolote.

Na ushauri yeye ndiye anaamua aupokee ama aukatae.

Kwa katiba hii atakuja kutokea rais ambaye ataamua:-
1. Kuzipiga marufuku na kuzifuta kabisa sherehe za Uhuru.
2. Kuulipua kwa mabomu na kuusabaza kabisa mlima kilinajaro .
3. Kuwauza na kuwaondoa kabisa wanyama toka hifadhi ya Serengeti na kugawa viwanja vya makazi.
4. Kubeba wanyama kwenda Unguja na waunguja wote kuwahamishia hifadhi ya Mikumi.

Kwa katiba yetu hii mtamfanya nini rais kama huyu?

Jamani katiba hii tuibadilishe.
 
Hayo mbona madogo. Hata akiamrisha watu wa mkoa flani wote wauwawe kisha mkoa huo tuufanye hifadhi ya mafuvu ya taifa linawezekana
 
Jeshi halitii kila Amri, mfano sasa hivi wakiamrishwa waishambulie USA watagoma hata kama ni huyo unayemuita Raisi wa sasa akitoa Amri.
 
Sherehe ni gharama kubwa, zifanyike angalau kila baada ya miaka 10
 
Halafu wale wakwapuaji wa mali za umma, ulaji wautoe wapi vile!???
 
hizo sherehe kwani zina faida gani? ni uharibifu wa fedha za uma tu.
 
Uzi unakichwa kizuri ila mwili na mkia hovyo kabisa.. Mtu anakwambia raisi aamue kulipua mlima.. sijui asimamishe sherehe.. bogus thinking kabisa.. sasa ndio nini.. kwahiyo tukikupa nchi utafanya ujinga huo?
Kiufupi huwezi hata uchukue uraisi na ukoo wako. Na katiba hihii.. na hata itokee wewe kama raisi ukaua mtu kwa mikono yako tukajua.. mimi kama mimi na rafiki zangu hata watano.. tutakuua kabla hujatuua na sisi.
Montalizard!!! Shubamiiiit!!!
 
Katika nchi yoyote kuna haya makundi matatu
1. Kuna raisi
2. Jeshi
3. Wananchi
4. Mataifa makubwa km USA
Kuwa raisi halafu vimba kichwa kuwa hakuna atakayekugusa.
Unamkumbuka Gadhafi, Kuruzinza, Mugabe na John?
Huyo anakosoa serikali, chapa risasi tu.

System yenyewe ni corrupt ndugu. Wengi wanaangalia maslahi ya matumbo na familia zao
 
Ndiyo! Hakuna la kumfanya, kwasabb katiba imesema rais hashitakiwi kwa jambo lolote.

Na ushauri yeye ndiye anaamua aupokee ama aukatae.

Kwa katiba hii atakuja kutokea rais ambaye ataamua:-
1. Kuzipiga marufuku na kuzifuta kabisa sherehe za Uhuru.
2. Kuulipua kwa mabomu na kuusabaza kabisa mlima kilinajaro .
3. Kuwauza na kuwaondoa kabisa wanyama toka hifadhi ya Serengeti na kugawa viwanja vya makazi.
4. Kubeba wanyama kwenda Unguja na waunguja wote kuwahamishia hifadhi ya Mikumi.

Kwa katiba yetu hii mtamfanya nini rais kama huyu?

Jamani katiba hii tuibadilishe.
Kwani atatawala milele
 
Back
Top Bottom