St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,956
- 5,149
- Thread starter
-
- #21
Kwa kweli somo zuri sana hili la kufungia mwaka sema 2 hapa kwa 4ne kidubwashika cha senks sikioni ila nimejifunza ki2
sijui ni kwanini katika ulimwengu wa mapenzi ni wachache sana wanaokubali kubeba lawama?wapenzi wengi wanapotofautiana au kugombana basi kila mmoja atamshutumu mwenzake kuwa ndio chanzo cha ugomvi huo,na wengine hufika mbali kabisa na kuanza kutangaza kwa watu kuwa yule bwana si lolote si chochote na ni mkorofi sijapata kuona,huyu naye atasema mwanamke gani yule mkorofi sijapata kuona,najiuliza kama wawili mnaopendana mkiamua kukaa chini na kumaliza tofauti zenu na penye makosa,mkosaji akakubali kubeba lawama itamgharimu nini?nimesukumwa kuwaza hivi kwa kilichomtokea jamaa yangu ambaye kwa sasa ni marehemu.alikuwa ameoa na kubarikiwa watoto wawili na cheo kikubwa kazini.lakini mke wake alijaliwa wivu wa ajabu,na mbaya zaidi katika usichana wake alikuwa championi wa judo katika chuo alichosomea,hivyo jamaa yangu kila akirudi kachelewa kidogo basi ni ngumi mtindo mmoja.kila wiki jamaa yangu alikuwa na kazi ya kununua fanicha mpya kufidia walizovunja,mwisho baada ya jamaa kuona nyumba haina amani akaamua kuwa mlevi.na kwa bahati mbaya akaharibika maini na figo hali iliyopelekea kupoteza maisha.na mke bado alimlaumu marehemu kuwa ulevi wake ndio umemuua asingeendekeza ulevi angekuwa bado hai.sasa katika mawazo yangu ninajiuliza kama wawili hao wangekuwa na maelewano mapema yote hayo yangetokea?msomaji nakuomba ujitathmini na kujiuliza,je uko tayari kubeba mzigo wa lawama ili kuokoa mahusiano yako?nawaza tu wakuu,asanteni kwa kunisoma na nawatakia wote mapumziko mema katika sikukuu hii inayokuja na heri ya mwaka mpya pia.
ukweli mtupu hapo paka.....
huo mfano wa huyo rafiki yako unatisha kwakweli
na mi nashukuru kwa kuuweka hapo kwani tumejifunza kitu ambacho tunafanya lakini huwazi kama inaweza kumpeleka mtu kubaya kihasi hicho..
uwi Paka harusi lini sasa....
na dhani umesha jua mengi kuhusu maisha.....😛arty:
Umesha wahi kuwaza ngono mzee?
Bado tunaenda mdogomdogo,mambo mazuri hayataki haraka mama.
safi......
nway maandalizi ya xmass yanaendeleaje??
Tunaendelea polepole mama,Si unajua X-mas zetu na winter ndo imekolea.
safi white x-mass napenda... sijawahi kuiona lakini..
ka baridi ikizidi karibu huku mtaa wa chini...
Ahsante sana pakamweusi, hilo ni tatizo kubwa sana kwenye ndoa nyingi au mausiano mengi,ila next time naomba usibold maneno yote, bold neno unalotaka kuweka msisitizo, pia weka paragraph ili mtu asichoke kusoma, enjoySijui ni kwanini katika ulimwengu wa mapenzi ni wachache sana wanaokubali kubeba lawama?Wapenzi wengi wanapotofautiana au kugombana basi kila mmoja atamshutumu mwenzake kuwa ndio chanzo cha ugomvi huo,na wengine hufika mbali kabisa na kuanza kutangaza kwa watu kuwa yule bwana si lolote si chochote na ni mkorofi sijapata kuona,huyu naye atasema mwanamke gani yule mkorofi sijapata kuona,najiuliza kama wawili mnaopendana mkiamua kukaa chini na kumaliza tofauti zenu na penye makosa,mkosaji akakubali kubeba lawama itamgharimu nini?Nimesukumwa kuwaza hivi kwa kilichomtokea jamaa yangu ambaye kwa sasa ni marehemu.Alikuwa ameoa na kubarikiwa watoto wawili na cheo kikubwa kazini.Lakini mke wake alijaliwa wivu wa ajabu,na mbaya zaidi katika usichana wake alikuwa championi wa judo katika chuo alichosomea,hivyo jamaa yangu kila akirudi kachelewa kidogo basi ni ngumi mtindo mmoja.Kila wiki jamaa yangu alikuwa na kazi ya kununua fanicha mpya kufidia walizovunja,mwisho baada ya jamaa kuona nyumba haina amani akaamua kuwa mlevi.Na kwa bahati mbaya akaharibika maini na figo hali iliyopelekea kupoteza maisha.Na mke bado alimlaumu marehemu kuwa ulevi wake ndio umemuua asingeendekeza ulevi angekuwa bado hai.Sasa katika mawazo yangu ninajiuliza kama wawili hao wangekuwa na maelewano mapema yote hayo yangetokea?Msomaji nakuomba ujitathmini na kujiuliza,je uko tayari kubeba mzigo wa lawama ili kuokoa mahusiano yako?Nawaza tu wakuu,asanteni kwa kunisoma na nawatakia wote mapumziko mema katika sikukuu hii inayokuja na heri ya mwaka mpya pia.
Ahsante sana pakamweusi, hilo ni tatizo kubwa sana kwenye ndoa nyingi au mausiano mengi,ila next time naomba usibold maneno yote, bold neno unalotaka kuweka msisitizo, pia weka paragraph ili mtu asichoke kusoma, enjoy