Naweza kuanzisha gazeti la udaku kwa mtaji huu?

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Ninataka kuanzisha gazeti la udaku ambalo nitalitumia kutangaza biashara zangu and all that. Nina ofisi na vifaa vyote vya ofisi, ninao vijana watatu ( wanafunzi wa uandishi wa habari chuo kikuu) ambao wapo tayari kufanya kazi na mimi kama waandishi wa kujitolea kwa muda wa miezi sita ( nitakuwa nawalipa allowances ). Ninataka kuwekeza mtaji wa shilingi MILIONI TATU kwenye hilo gazeti. Shilingi Laki Tano ( Gharama za kusajili gazeti ), shilingi milioni moja, gharama za kuprint nakala za magazeti ( Nitakuwa ninatoa nakala elfu moja kila wiki ) nakala moja hutolewa kwa shilingi 220, so nakala elfu moja kwa wiki zitanigharimu shilingi LAKI MBILI NA ELFU ISHIRINI kwa wiki, hiyo pesa nyingine nitaitumia kuendeshea ofisi.. Ninaomba ushauri na mawazo kwa mtu yoyote ambaye ni mdau wa magazeti. Asanteni sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…