Naweza kujenga nyumba ya kisasa kwa mil 20?

fiksiman

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2008
Posts
402
Reaction score
107
Naomba ushauri nina mtaji wa mil 20, tayari nina kiwanja cha kutosha tu. Je naweza kujenga nyumba nzuri ya kisasa kwa mtaji wa mil 20?
 
Nyumba ya kisasa maana yake nini? Ujue kuna mtu kwake nyumba ya kisasa pesa hiyo inamaliziwa kwenye tiles tu!

Lakini kama unazungumzia nyumba zetu za kawaida huku mitaani, kwa mfano 3 bedroomed self contained house (+sitting room and kitchen) - yamkini ni kwamba utapaua. Utanza pia finishes lakini hutazimaliza.
 

angechanua vizuri muundo wa nyumba anayoiota yeye kwa hiyo hela
 
mkuu The Boss tafadhari njoo umsaidie kijana hapa!
 
Last edited by a moderator:
Kujenga utajenga tatizo utajenga ya namna gani
 
Very helpful link Mkuu, sikujua kama kuna wadau walishajadili hili jambo kwa marefu. I hope Mod ataihamishia hii thread kwenye hili thread ya zamani

nakutakia mafanikio mema kiongozi
 
Naomba ushauri nina mtaji
wa mil 20, tayari nina kiwanja cha kutosha tu. Je naweza kujenga nyumba
nzuri ya kisasa kwa mtaji wa mil 20?

mkuu kamwe hauwezi, hiyo pesa fanyia biashara. Au uanze ukitambua kuwa utafika mahali.. usimame ujipange kwanza.

pesa hiyo hauwezi kufika hata katika level ya madirisha. Msingi tu utakuja kutuambia, na inategemea sana na kiwanja chako kiko level ama la!
 



Hebu pitia vizuri hesabu zaku mkuu!!!!!
 
Naomba ushauri nina mtaji wa mil 20, tayari nina kiwanja cha kutosha tu. Je naweza kujenga nyumba nzuri ya kisasa kwa mtaji wa mil 20?

mkuu miruzi mingi ilimpoteza mbwa,we anza nayo tu hata kama haitotosha lakini nyumba itafika mbali ambapo utaweza kumalizia kidogo kidogo ila itabidi usimamie mwenyewe kila hatua hapo nyumba itakua mbali,
 

Inategemea na aina ya nyumba na eneo but kwa nyumba ya kawaida(vyumba 3) itaisha kitakachobaki ni finishing tu
 
nyie ndo mliotajirisha mafundi
 
Hii inawahusu wale waliowahi kujenga nyumba ngoja mie nipite kimya kimya
 
Naomba ushauri nina mtaji wa mil 20, tayari nina kiwanja cha kutosha tu. Je naweza kujenga nyumba nzuri ya kisasa kwa mtaji wa mil 20?

Unaweza. Cha msingi ni eneo la ujenzi likoje , tambarare, mabonde, lina maji, aina ya udongo n.k
Nipm nikushauri!
 
Me nakushauri kuanza ujenzi soon na nina iman kwamba utafika mbali sana hata kama hutafanya finshing no matter
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…