Naweza kukata rufaa nikilazimishwa kufanya mtihani Sikukuu ya Uhuru 9/12?

Naweza kukata rufaa nikilazimishwa kufanya mtihani Sikukuu ya Uhuru 9/12?

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Vyuo vya afya vimepanga ratiba ya mithani hadi siku ya siku kuu ya kiserikali.

Vyuo hivi vina watumishi wa umma pia ambao kwa namna moja ama nyingine wanayo majukumu katika siku hii maalum ya kusherehekea Uhuru wa Tanganyika.

Kwanini hawa wanaopanga kazi siku kama hii wasichukuliwe hatua kwa kudharau sheria ya nchi maana ni watumishi wa serikali?

Je, ninaweza kukata rufaa kupinga maamuzi yoyote yatakayotolewa dhidi yangu kwa kukataa kufanya mtihani siku hii?
 
Vitu vingine puuzia.

Hakuna cha maana ulichopanga kufanya siku hiyo ya mtihani.

Sawa, unaweza kushinda ila kwa majuto. Hujafanya mtihani, umekaidi. Discontinued!.

Unakuja kushinda baada ya miaka miwili. Sasa umeshinda nini? Upuuzi tu.
 
Back
Top Bottom