Naweza kukumbuka vizuri tu yaliyofanyika nikiwa umri wa miaka mitano

Naweza kukumbuka vizuri tu yaliyofanyika nikiwa umri wa miaka mitano

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Wewe je?

Kumbukumbu zako zimeanzia ukiwa na umri gani au tukuache kwanza?

Wakuu msiwachukulie poa hawa madogo na msitende mambo hasi mbele yao ukidhani wanasahau mapema kuna umri ukifika mtoto hasahau kamwe.
 
Kumbukumbu zinategemea mtu na mtu na tukio kwa tukio. Matukio makubwa ya huzuni na furaha huwa hayatoki kirahisi. Kwa umri nafkiri wengine huanzia mapema sana from age 3/4
 
Huwa nakumbuka nikiwa na umri huo niliwahi kuambiwa 'hapa sio kwenu' plus nikatandikwa kofi zito sana kisa tu niliomba soda, ni miongoni mwa matukio ambaya kila nikiyakumbuka huwa naona ni kama limetokea muda mfupi uliopita, ila nilishasamehe
 
Ni vingi tu navikumbuka lakini kubwa kuzidi, nimepata uwezo wa ku-imagine nikiwa na miaka nane, kujenga picha akilini ya matukio.

vitu navyokumbuka nikiwa na miaka mitatu hadi mitano:
  • Nakumbuka nilikuwa sipendi maziwa napenda chai ya rangi
  • Nakumbuka siku napelekwa kuanza shule nililia sana nilipoachwa shuleni.
  • Nakumbuka niliwahi kuchoma fensi ya mabua ya bustani, enzi hizo nilidhani ni shamba.
  • Nakumbuka siku ambayo nilipata mdogo wangu tuliepishana miaka mitatu (rip)
  • Nakumbuka siku ambayo kaka hakulala nyumbani alienda kusherekea mwaka mpya alishushiwa kipigo asubuhi
  • Nakumbuka kuna siku niliumia nikawekewa chumvi kwenye kidonda.
  • Nakumbuka kwa mara ya kwanza naona mtu kalewa anapepesuka, alikuwa houseboy anaehudumia ngombe
  • Naukumbuka mchezo wa baba na mama tunajifanya tumekuwa wazazi, itoshe kusema ni mchezo mbaya.
  • Namkumbuka paka wa nyumbani alipenda sana kuwa karibu yangu
  • Nakumbuka jina la mbwa wetu, sitaliweka hapa maana kuna watu wanaitwa hivyo
 
Ninakumbuka tukio ambalo lilitlkta nikiwa na umri wa miaka 3
Ulikuwa ugomvi mkubwa baina ya mama na marehemu baba, .mzee alipigwa chupa ambayo ilimuumiza sana. Na bahati mbaya sisi watoto tukawa tuko upande wa kumtetea mama.
Kadiri ninavyokuwa baba nimekuja kufahamu kuwa mzee alionewa sana kipindi cha ugomvi ule, Angelikuwa Hai ningemsemesha kitu cha kumfariji.
 
Back
Top Bottom