Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimesoma sehemu kuwa mmea huo una protini nyingi kwa kulisha mifugo, hasa wanyama wanaocheua.
Sijaona sehemu wanapoelezakuhusu wanyama wengine.
Je, inafaa pia kwa kulisha nguruwe na akapanufaika kwa protini iliyomo?
Asante sana.Nguruwe pia anaweza kunufaika na protein inayotakana na leucaena tena wanazipenda kwel kwel
Asante sana.
Niwalishe kwa kiwango (kipimo) gani?
Niwape kadiri nipendavyo/ninavyoweza kupata?
Asante sana kwa ushauri na maelezo muruwa.Usiwalishe zaidi ya 10% ya total feeds per day kulisha kiwango kikubwa inamadhara kutokana na chemical iitwayo mimosine inayopatikana kwenye leucaena.
Japo kuna njia za kupunguza hio chemical kwenye hayo majani kama kuyakausha then unayachanganya na vyakula vingine kama pumba na mashudu .
leucaena offcoz ni nzuri inaviwango vingi vya lysine methionine ,thionine ,madini na aina nyingine za amino acids unaweza kutumia kwenye kama mbadala wa soya hivo kupunguza gharama za kulisha wanyama wako na ukapata matokeo mazuri tu
Asante sana kwa ushauri na maelezo muruwa.
Umenifaidisha mno.