Kwetu sisi tulofanya biashara ya kahawa pale kahawa House Moshi, lazima kila mzigo uonjwe, si rahishi kusadiki maneno yaliyoandikwa kuhusu mzigo husika. Lazima tuonje, kama kuna ki-ladha cha udongo, vitunguu, samaki, dagaa au uchachu. Ukisharidhika kuwa mzigo uko poa, basi una-bid na kama ni mzuri sana, unaongeza dau ili ushinde bidders wengine.
Kwa hiyo kuonja ni utaratibu wa kawaida tuu ili ufanyapo uamuzi, uamuzi huo uwe ni evidence-based. Hizi habari za ooh, kuonja ni dhambi, ooh ni kinyume na maadili, ni njama za kuficha na kunyong'onyesha ukweli. Karibu katika ulimwengu wa uonjaji.
Capita