Naweza kupata control number Kwa ajili ya kulipa makadirio ya Kodi ya biashara

lutajangurwa

Senior Member
Joined
Sep 21, 2019
Posts
126
Reaction score
172
Naomba kufahamishwa na yeyote anayejua namba ninavyoweza kupata control number Kwa ajili ya kulipa makadirio ya Kodi ya kampuni yangu? Je ni lazima kwenda TRA Kila tarehe inapowadia? Je inawezekana kupata online? Msaada plse
 
Inawezekana kupata online mkuu, ulivyokadiriwa si ulipewa namba inaitwa "Debit no"Kwa kila quarter? If yes basi unaweza kulog in TRA home page utaenda sehemu ya domestic payment, then assessed Tax itakuambia uweke hiyo Debit no na details zingine, utaona kiasi exactly ulichokadiriwa ,utaconfirm and submit , hapo hapo utaletewa control number.
 
Tena usichelewe kuepuka penalty kesho tar 30 ndiyo mwisho, na network inakua busy sana sababu ya deadline, leo tangu asubuhi ilikua inasumbua, you can't even login ama utalogin ila kwa mbinde sana
 
Dawasco wako kisasa kuliko Tra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…