Naweza kupata wapi tafsiri ya Kiswahili ya sheria za Tanzania

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Posts
3,173
Reaction score
482
Wana Jamii habari za siku njema ya leo
Naomba wataalamu wa sheria wanisaidie hapa. Mzee wangu kanunua kashamba kadogo kijiji fulani hivi. Kwa kuwa aliyemuuzia ni swahiba wake walilipana mbele ya familia na wakakabidhiana hati za kumiliki kimila. Wazee wetu hawapendi usumbufu sana. Siku zikaenda na akawa anawapa ndugu wanalima na shughuli mbalimbali. Ni juzi tu Mwenyekiti wa kijiji kauziana na jamaa fulani kwa kushirikiana na mtoto wa mmiliki wa awali. Kuuliza anaambiwa kwa Sheria Za Ardhi namba 5 ya mwaka 1999 kifungu cha 30 (3) na (6) mauziano yao hayakuwa halali. Sasa nimejaribu kutafuta hiyo sheria sioni mahali imechapishwa. Hebu nisaidieni inapatikana wapi na kwa lugha nyepesi niweze kumsaidia mzee wetu. Natanguliza shukrani

EM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…