Naweza kusoma Master of Arts, kama sikuisoma kwenye Bachelor?

Naweza kusoma Master of Arts, kama sikuisoma kwenye Bachelor?

Afande Nyati

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
2,385
Reaction score
1,414
Habari zenu wana JamiiForums, Poleni na majukumu ya kila siku..... naomba kuuliza kama kuna uwezekano wa kusoma MA wakati ni tofauti na degree ya kwanza niliyosomea?
 
Habari zenu wana JF, Poleni na majukumu ya kila siku..... naomba kuuliza kama kuna uwezekano wa kusoma MA tofauti na degree ya kwanza niliyosomea.....

ndiyo. hadi unamaliza digrii ya kwanza hukulifahamu hilo?au ndo unajiandaa kuanza bachelor?
 
Sio zote unaweza samo, mfano MA upende wa Afya, lugha, elimu, kilimo, aridhi, uhandisi na computer hauruhusiwi kusoma MA kama degree ya kwanza hujasoma course husika au yenye uhusiano, ila social science courses mara nyingi hazina masharti
 
Inategemea ni degree ipi na unataka kusoma chuo ipi, ungefunguka zaidi
 
Inategemea ni degree ipi na unataka kusoma chuo ipi, ungefunguka zaidi

Nimesoma degree ya political science na public administration mkuu, nataka niendelee na masuala ya uchumi je itawezekana hata kwa kupitia post-graduate...........
 
Kwa UDSM huwezi
Unahitaji background nzuri ya hesabu
uchumi ina hesabu nyingi sana
kwa mtu wa PSPA itakusumbua kama hujasoma Adv. Maths
 
Nimesoma degree ya political science na public administration mkuu, nataka niendelee na masuala ya uchumi je itawezekana hata kwa kupitia post-graduate...........

Hebu nijuze kwanini unataka ukasome masters ya uchumi...?
Je wewe ni muajiriwa unataka ukaongeze ujuzi...?
Au umemaliza degree mtaani pagumu na ajira hakuna...?
Nifahamishe tafadhari...!!!!
 
Hebu nijuze kwanini unataka ukasome masters ya uchumi...?
Je wewe ni muajiriwa unataka ukaongeze ujuzi...?
Au umemaliza degree mtaani pagumu na ajira hakuna...?
Nifahamishe tafadhari...!!!!

Mr. Karim inaonekana una mawazo mazuri ambayo yatanipa mwanga nakotaka kwenda... Tunaweza tukawasiliana private please, naona itakuwa nzuri sana
 
Back
Top Bottom