Nashawishika kukushauri sababu nilisoma CBG pia late 1990's (ni muda kiasi sasa na ushauri wangu waweza kukosa dondoo za hali za sasa).
CBG ni combination nzuri sana. Ipo katikati ya science na arts/social science. Ukifaulu vizuri waweza jiunga na coz nyingi tu vyuo vikuu.
Mimi nilisoma BScwGY (Geoloy/Geography double major...unatunukiwa ugeologist). Waweza kusoma pia coz kadhaa pale idara ya botany (udsm), hata BSc .wildlife unachukuliwa. Ipo BSc. General Science (sijui kama bado ipo), Environmental Science, etc, etc. Nyingi tu ilimradi ufaulu vizuri.
Mifano yote hapo juu ni kwa udsm bado kuna vyuo kama SUA wana kozi kadhaa za kilimo na mifugo unaweza dahiliwa.
Kipindi fulani ungeweza kusoma Medicines KCMC ila sasa sijui. Wakati wangu udahili pale ulizingatia ufaulu kwenye Biology na Chemistry. Chaguo ni lako tu.
Ila angalizo (japo ni mapema sana kukushauri hili), mafanikio maishani hayajalishi ulisoma kozi wala chuo gani. Ni namna tu utakavyojiandaa/utakavyoandaliwa kutumia hiyo platform kupambana na maisha. Usisome ili uajiriwe bali uajiri! Kila la heri.