Dah! Jaribu kwanza kujifunza virus nini, kuna aina kibao za virus mpaka sasa; kila moja ana misheni tofauti anapofanikiwa kuingia katika mashine yako na kulingana na alivyoagizwa na mtengenezaji! Unapoongelea "madhara"-kile kitendo cha kuvamia mashine ya mtu na kuanza kuiagiza ifanye vitu tofauti na matakwa ya mmiliki tayari hayo ni madhara!!! Najua hauna knowledge yoyote ya programming, lakn sijajua wewe unataka kutengeneza "chumaulete" la kuchuma vitu gani, yaani malengo yako hasa ni nini!
Ingekaa vizuri zaidi kama ungeuliza " Computer Virus ni nini, na madhara yake ni nini katika computer?"
Naamini ungepata maelezo ya kina kutoka kwa wabobezi wa mambo hayo, wamejaa kibao humu ndani utawaona tu!