Naweza pata mkopo bank kwa dhamana ya nyumba isiyo na hati?

YUSHIN

Member
Joined
Feb 11, 2012
Posts
59
Reaction score
7
Wadau hivi inawezekana kupata mkopo kwenye mabenki esp. NMB na CRDB kwa dhamana ya nyumba isiyo na hati? ila hiyo nyumba ipo kwenye kiwanja kilichopimwa na kina offer/leseni ya kiwanja.
Msaada kwa wenye ufahamu
 
Unaweza kupata mkuu,chamsingi barua ya uthibitisho wa umiliki wa kiwanja(hati ya kimila) pamoja na barua ya mtendaji au mwenyekiti wa mtaa kukutambua kama mkazi na mmiliki wa kiwanja,wanakuja kuitazama nyumba then taratibu nyingine za kupata mkopo zinafuata.
 
asante mkuu
 
Ila uwe makn na hzo pesa eeh ucjerudia nyumba za kupanga
 
Mkopo unapata, ila elekeza kwenye kusudio kwa uaminifu na kuzingatia ratiba ya rejesho unatoka
 
Unataka kuweka nyumba bond? Karibu kwenye kupanga tena
 
Ila uwe makn na hzo pesa eeh ucjerudia nyumba za kupanga
Umempa angalizo la Msingi...!
Wengi wamerudia walikotoka, kama kwamba, pesa kutoka taasisi hizi (Mabenki) zina Laana...!
 
Crdb na nmb hamna kitu kama hicho
 
Nyumba isiyo na hati ni kama kiberiti au Uyoga. Huwez pata labda uende Tanzania woman bank
 
Ukichukua hiyo hela unakaribia kuwa mpangaji,sijawahi kusikia mkopaji kaenda benki na kukomboa hati yake.
Mkopo wa benki ni shimo ndefu ukiingia huko hutoki ndugu yangu, lugha itabadilika utaanza kuambiwa neno top-up hapo biashara yako itakuwa imeisha jumla, juzi nasoma gazeti kuhusu nakumatt inasikitisha sijui mikopo ni laana.
Nakuomba tu ukisikia mkopaji aliyeweza kutoa hati yake benki unijulishe. .
 
Mkuu why only CRDB and NMB ? Kuna zaidi ya Bank 30 Tanzania na zote zinafanya landing business kwa gharama nafuu na mashariti mepesi kabisa.
 
Nilisikia Access wanakubali ukiwa na property hata isiyo na hati
 
Wadau hivi inawezekana kupata mkopo kwenye mabenki esp. NMB na CRDB kwa dhamana ya nyumba isiyo na hati? ila hiyo nyumba ipo kwenye kiwanja kilichopimwa na kina offer/leseni ya kiwanja.
Msaada kwa wenye ufahamu
Mkuu habari,
Taasisi nyingi za kifedha hawakubali kutoa mkopo kwa dhamana ya nyumba isiyo na hati. Kuna baadhi hata leseni za makazi hawakubali kuzipokea kwa kigezo kuwa inawezekana unayo leseni ya makazi ambayo uliipata kwa wakati fulani lakini baadae ukapata hati kamili
Nakumbuka kitambo lakini Accessbank walikuwa wanakubali leseni za makazi na hati vilevile lakini ilikuwa muda kidogo sijajua kwa sasa
Ila kwa mkopo kama sio mkubwa hadi mil 6 hivi kwa leseni ya makazi au hati za kimila SIDO wanakubali. Nakushauri jaribu huko lakini lazima uwe na biashara!
Ushauri
Mkopo kama ukipata jitahidi kuiheshimu hiyo pesa na itumie katika malengo uliyojiwekea, kushindwa kulipa deni ni hatari kwa mali yako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…