Naweza pata wapi Camping Hammock

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Nimeona niombe msaada kupita group hili la wajuzi wa mambo
Nilikuwa nataka kujua mahali au maduka ambayo naweza pata Camping Hammock kwa Mwanza,Dar au hata mikoa mingine.
Na je kama ipo inaweza kuwa ni bei gani
Nawakilisha kama picha ilivyo hapo chini
 

Attachments

  • Hammock.png
    895.5 KB · Views: 5
Nenda Ngerengere jeshini.
 
Subiri niweke kambi hapa.
Maana nikiwahi kuziona kikuu, lakini mchina simuamini kabisa
 
Kuna jamaa anauza zile portable kwa 150k
 
Mkuu siutengeneze mwenyewe?utotoni tulisuka hizo Kwa nyavu na katani ila kwakuwa ushakuwa mbaba kuliko uuziwe hicho kituko Bora utengeneze mwenyewe la msingi kitambaa kiwe kigumu.
 
Mcheki Camp with Jackie 0752232101 yupo Mwanza anazo Hammocks na stand zake bei zinarange kwenye 150k
 
Kuna jamaa anauza vtu used anatoa mara nyingi Uturuki, uwa naziona Sana japo hazkaagi sana...
Maeneo ya kijichi
 
Mcheki Camp with Jackie 0752232101 yupo Mwanza anazo Hammocks na stand zake bei zinarange kwenye 150k
Aisee vvm nakushukuru mno mno jana nimempigia Jackie nimeongea naye kwa kweli nitachukua kwanza hizo zenye stand hii hammock ya kutundika mtini nitatafuta taratibu.
Niko Mwanza itakuwa rahisi
uzuri wa hii kitu kwa dar kukiwa na joto sana ndani unaweza simika hii kitu nje kwako chini ya mti ukapumzika hata kama ni usiku ili mradi uwe sehemu isiyo na vibaka.
Pia ukienda msibani unaweza kwenda nayo ukaifungua ukalala
Pia kuna member Vito Corleone amenishauri nitengeneze ya kienyeji nitatafuta fundi wa kusuka nyavu nene anaisaidie
Nataka home kwangu pawe kama beach hakuna haja ya kwenda beach
Uzuri wa JF ndio huu sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…