Kama wewe ni mmiliki wa hiyo site maana yake ina malware au virusi, mara nyingi ni kutokana na watu kuhack site hasa za wordpress na kupachika malware.
So wewe kama mmiliki inabidi urudishe site yako kwenye hali nzuri kisha uwataarifu Google hiyo warning itatoka baada ya siku kadhaa.
Nenda
Google Transparency Report kwa kuaanza itafute site angalia tatizo ni nini.
Rekebisha tatizo.
Kisha jiandikishe Google Search console
Google Search Console
itakupa hizi warning mapema kama mmiliki na itakuwezesha kusubmit site yako kama umefanya marekebisho.
Kwenda mbele halikisha unatumia passwords ambazo ni secure na unafanya update ya wordpress na plugins mapema.