Nawezaje kubadiri hobby hii kuwa biashara

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,363
Reaction score
1,431
Wasalaam great people
Ladies and gentlemen

Kuishi kwingi kuona mengi. Hakika tunaishi katika dunia amabayo tunaanza kuona watu wenye vipaji au hobbies zoa wanazigeuza kuwa biashara na hakika baadhi yao wanatoka kimaisha.

Leo tuna wanamziki, wacheza mpira, wachoraji na hata wana mitindo maalufu na wanaongoza familia zao kwa matunda ya vipaji vyao.

Kwa muda mrefu, niwe nimelala, niwe natembea, niwe ofsini na pengine hata nikiwa kanisani , kitu ambacho huwa kinakuja kwenye mind yangu ni UPENDO

Napenda kuona watu wanapendana, napenda kuona watu wanafanya matendo ya hisani kwa jamii za wahitaji, napenda kuona watu wanasameheana na kumaliza changamoto zao, napenda kuona tabasamu katika nyuso za wengi, napenda kuona kujaliana na mashirikiano baina ya watu na hata vikundi. Kifupi matendo yote ya upendo yametawala Ufahamu wangu

Kwa mkutadha huo najitokeza kwenye ukurasa huu ili nipate mchango wa mawazo ni kwa jinsi gani naweza geuza hobby hii ya kupenda Upendo utawale kuwa business idea?

Nataka utashi huu wa ndani na hulka iliyokwisha jengeka ndani yangu kuwa wazo la kibiashara ili linisaidie kufanikisha maisha yangu, coz najua Mungu hajanipa mguso huu wa tofauti ili niukalie tu pasina kutumika.

Kwa heshima ya forum, hii ambapo najua sitotoka bila mawazo chanya, hivyo natanguliza acknowledge zangu

Regards
 
Kongole kwa kutambua nini unapenda zaidi kufanya katika maisha yako.
Sasa ushauri ni jitahidi kuwa mshauri wa masuala ya mahusiano ya "kijamii na afya ya akili" ("social and mental health counselor) lakini jiboreshe zaidi kwa kuongezea ujuzi kwa kusoma vitabu mbalimbali vya saikolojia na kama una nafasi, umri na uwezo unakuruhusu unaweza kujiendeleza zaidi kimasomo katika level mbalimbali za kielimu
Ukiachana na kujiendeleza, vlvl upande wa pili wa shilingi, jitahidi kujijenga jina la huduma, ktk semina mbalimbali jitahidi kuomba nafasi japo kwa muda mfupi unakuwa unaandaa maelezo yk ya huduma yenye mvuto, jirekodi video fupi japo za dakika 1, ukizungumzia jambo mfano, kwa nini tusamehe, umuhimu wa mahusiano mema, hatari ya kuwa na chuki, utapambana vp na "stress"! Taratibu utaanza kuibuka hatimaye kuanza kuvuna mapato kutokana na hobby ambayo utaigeuza kuwa fursa
 
Vizuri kbsa na kpaj chako ni kizur na kinahtaka sana kwenye dunia ya leo, binafsi najijua ninapenda sana utani, yan sana kwa maneno napenda sana kumfanya mtu acheke. Ili nitumie hio kama fursa inabd niwe comedian, tatzo mwonekano wa kicomedia sina kbsaa na siko interested, popote ninapoish najulikana kwa utani, humu jf kuondoa nyuzi zangu sijawah comment kitu cha serias bla kuweka utani, Napenda sana utani weng humu wananiambiaga niwe comedian ila siwez nitatumia vipaj vngne kama fursa hk nitakitumia mtaan. Yote kwa yote lengo n kufanya dunia kua sehemu ya furaha, aman na upendo.
 
una mawazo kama yangu sema me tatizo ni muda tu ni text pm tukutane tuongee kama upo Dar es salaam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…