Ukifuatilia historia ya dunia utaona bila shaka kuwa Walimwengu wamechanyikiwa siku zote. Vita kila kona ya dunia, mauwaji, majanga, visa vya kutisha, uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira, wizi na mengineyo.
Kuishi katika dunia ya namna hii inahitaji uwe na ufahamu wa aina yake. Uwe na uwezo wa kujitengenezea furaha hata kama mambo hayaendi unavyotaka.