Japo muda umepita sana ila itasaidia na wengine wengi,
Hapo kuna mzingira mawili tofauti ambayo ni muhimu kuyafahamu vyema.
Mazingira ya kwanza ni ya wakili kutokomea bila kufanya huduma husika, hapo kama ulifanya malipo na unao udhahidi itakuwa rahisi zaidi kwako, hapo utaweza opt ama kesi ya madai au kwenda kwenye Kamati ya maadili ya Mawakili hapo utatoa lalamiko lako, ila uwe na maelezo yamenyooka.
Mazingira ya pili ni mtu sio wakili ila anajinabaisha kama wakili, hapo kuna jinai kama atakuwa anatumia jina au taarifa za wakili yoyote, pili kuna madai kama ulishalipa tatu kuna Chama cha Mawakili (TLS) nne Kwa msajili wa Mahakama Kuu. Popotekati ya hapo utapata msaada mzuri.
Ila ni vyema san jamii ikafahamu tofauti kati ya Wakili na Mwanasheria na pia jamii iepuke sana kufanya kazi na mtu asiyena ofisi maalumu.
Wakili ni mtu aliyeorodheshwa kwenye orodha ya mawakili na kupatiwa namba ya orodha, anayeweza kumuakilisha mtu ama Mahakamani au katika vyombo vingine vya utekelezaji wa sheria
Mwanasheria ni mtu aliyesoma shahada ya kwanza ya sheria. Hapo utaona ni mtu aliyesoma shahada ya sheria na sio diploma wala cheti hao sio wanasheriahao ni wasaidizi wa sheria. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya msaada wa kisheria.
Mwanasheria asiye Wakili haruhusiwi kumuwakilishamtumahali popote kama mwanasheria wake/wakili wake, vile vile haruhusiwi kuandaa nyaraka zozoteza kisheria zinazokwenda Mahakamani.
Nadhani itawapa wadau mwanga